Mstari mweusi kwenye tumbo

Mstari mweusi kwenye tumbo

OCC Doctors

Senior Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
114
Reaction score
172
'Linea nigra' (mstari mweusi"), ambao mara nyingi hujulikana kama mstari wa ujauzito, kwa kawaida unaoonekana kwenye tumbo. Ni mstari unaopita wima katikati ya tumbo kutoka eneo la chini hadi kwenye kitovu, lakini pia unaweza kujitokeza kutoka eneo la chini hadi juu ya tumbo. Kwa wanawake wajawazito, mstari huu unahusishwa na kuongezeka kwa homoni yenye kichocheo cha melanocyte iliyotengenezwa na kondo la nyuma (placenta), ambayo husababisha weusi wa mstari huo na ndio husababisha weusi wa chuchu kwa mjamzito. Linea nigra kawaida hupotea ndani ya miezi michache baada ya kujifungua.

170254876-56a770fc5f9b58b7d0ea8724.jpg
 
Doctor mimi mbona sijawahi kuzaa ninao huo mstari unaishia kitovuni tena umekolea tangu najitambua kabla hata sijabalehe.. una maana gani
 
Doctor mimi mbona sijawahi kuzaa ninao huo mstari unaishia kitovuni tena umekolea tangu najitambua kabla hata sijabalehe.. una maana gani
Utakuwa na tatzo la melenocytesisy. Ina madhala kwa badae, nipm nikusaidie
 
Hata kama nmezaliwa nao?
Kuwepo kwa mstari wa ujauzito mara nyingi inaonekana kama shida ya mapambo tu (cosmetic problem) lakini kiuhalisia hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwa sababu haina madhara. Mstari huo unaweza kuonekana kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha melanin kwenye seli za ngozi, katika hali nyingine, wale ambao wana mstari huo lakini bado hawajapata ujauzito, ugonjwa wa PCOS na ugonjwa wa Addison ndio huwa sababu inayoweze kupelekea kuwepo kwa mstari huo. Daktari wako atakueleza zaidi sababu tofautitofauti ikiwa hauna matatizo hayo hapo juu.
 
Madhara gani mbona me ninao toka binti na sijawahi hata kupata mtoto?
Usijali ni hali isiyo na maudhi, lakini pia sababu zingine ambazo linea nigra inaweza kuonekana kwenye tumbo lako bila kuwa mjamzito ni pamoja na matumizi ya njia mbalimbali za uzazi wa mpango (birth control), ukosefu wa adrenal (Adrenal Insufficiency or failure) , kuvurugika kwa vichocheo mwilini (Hormonal Imbalance), pia huweza kutokea ikiwa wewe ni mwembamba sana au unafanya kazi nyingi zinazoshughulisha tumbo.
Daktari wako atafahamu zaidi
 
Dr mimi nina umekolea haswa na nina watoto 3!
Linea nigra kawaida hupotea ndani ya miezi michache baada ya kujifungua. Kwa kipindi cha muda wa mwaka mmoja, mstari utaendelea kufifia. Unaweza ukawa huupendi kutokana na njia ambayo mstari unakufanya uonekane ukivaa mavazi ya urembo wa kitovu, au ukiwa ufukweni. Japo wengine hutumia mafuta ya cream kuuwondoa hali ambayo siyo nzuri kiafya, Lakini ni bora kuruhusu ufifia wenyewe. Na ikishindikana kutoweka unaweza kuiacha tu na ikawa ni moja ya nembo ya heshima kama kumbukumbu ya kujiunga na klabu ya wazazi.
 
Hata wavulana hua wanao, ila wakikua na kuwa wanaume huwa unapotea nadhani
Ndio Linea nigra inaweza kujitokeza kwa baadhi ya wanaume wanaofanya kazi nyingi zinazoshughulisha tumbo (kama vile kwa baadhi ya wanaofanya mazoezi ya kuongeza six pack), pia wakati mwingine inaweza ikatokea kwa wazee zaidi ya miaka 50 ambao wameathirika na maradhi ya tezi dume.
 
Doctor mimi mbona sijawahi kuzaa ninao huo mstari unaishia kitovuni tena umekolea tangu najitambua kabla hata sijabalehe.. una maana gani
Kwa uelewa wangu mdogo huo ni moja ya misuli.
Mwanamke awapo mjamzito huwa mweusi zaidi kutokana na kwamba mtoto alieko tumboni anavozidi kukua anakua kama anaupush kuelekea nje ambapo huonekana zaidi. Ndomama mimba ikiwa ndogo hauonekani sana tofauti na ikikua. Pia anapojifungua weusi hupungua



Cc Smart911
 
Sasa mimi ninao tangu zamani hata miaka 15 sasa kabla hata sijabalehe sina mtoto na sijawahi hata kupata mimba
ndio nauliza ina maana gani

Kwa uelewa wangu mdogo huo ni moja ya misuli.
Mwanamke awapo mjamzito huwa mweusi zaidi kutokana na kwamba mtoto alieko tumboni anavozidi kukua anakua kama anaupush kuelekea nje ambapo huonekana zaidi. Ndomama mimba ikiwa ndogo hauonekani sana tofauti na ikikua. Pia anapojifungua weusi hupungua



Cc Smart911
[
 
Back
Top Bottom