Mstahiki Meya wa Kinondoni aendelea kuchanja mbuga

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Diwani wa kata ya Ubungo ambaye ni mstahiki meya wa manispaa ya kinondoni wa sasa Mh Boniface Jacob ameonekana kuwa na kasi ya ajabu katika utendaji wake wa kazi ya kuwatumikia wananchi wa manispaa ya kinondoni amedhihirisha kuwa ni kiongozi wa mfano wa kuigwa.

Toka alipoaza kuwatumikia wananchi wa manispaa hiyo ya kinondoni amekuwa akifanya kwa vitendo na si kwa maneno au blabla. Ni imani yangu kuwa kama mameya wa manispaa nyingine zote nchini na wenyeviti wa halmashauri zote na viongozi wengine waliopewa mamlaka ya kuongoza wananchi wakiamua kufuata nyayo za Mh. Boniface Jacob basi tutaishi kama wafalme nchini hapa. Kwa kasi hii hakika Boniface anaendelea kutuelimisha na kutubadilisha kifikira kwamba tunahitaji mabadiliko ya juu karibu nchi nzima.

Hivi karibuni mstahiki meya bwana Mh Boniface Jacob aliwatangaziwa wananchi kuwa bajeti ya mwaka 2016/2017 itawawezesha wananchi kupata huduma bure za afya pia alisema watapata mikopo itakayoweza kuwainua kiuchumi na ameonesha mikakati mbalimbali ya kuwaendeleza wananchi ili wanufaike na raslimali zao.

Juzi tr april 20, mh Boniface alifanikiwa kusaini mkataba na kampuni ya MS/H. P GAUFF INGENIEURE GMBH&CO, KG-JBB ambayo itatoa huduma za ushauri (CONSULTANT SERVICES) katika usimamizi wa ujenzi wa miradi ya DMDP(DAR-ES-SALAAM METROPOLITAN, DEVELOPMENT PROJECT) itakayotekelezwa katika manispaa ya kinondoni. Mradi huu utasaidia kupunguza au kuondoa kabisa foleni na mafuriko kinondoni hapo. Akizungumza na mwandishi wetu mh Boniface anasema"Foleni, mafuriko yatabaki kuwa historia ya manispaa ya kinondoni...... naahidi kuwatumikia wananchi wangu usiku na mchana kwa moyo wangu wote" mstahiki meya amedhamiria kuwatumikia wananchi ili wasijute kuchagu UKAWA anatamani wananchi wote wanufaike na raslimali zao.
Leo alikua kwenye utoaji wa hela za mikopo kwenye vikundi mbalimbali
 

Attachments

  • IMG-20160422-WA0034.jpg
    IMG-20160422-WA0034.jpg
    95.9 KB · Views: 24
  • IMG-20160422-WA0035.jpg
    IMG-20160422-WA0035.jpg
    85.6 KB · Views: 24
  • IMG-20160422-WA0036.jpg
    IMG-20160422-WA0036.jpg
    87.2 KB · Views: 25
Mimi ni ukawa damu, huo mradi waliopata Gauff wakishirikiana na Nimeta Consult ni mradi ambao mchakato wake ulianza mda mrefu sana, hata sidhani kama alikuwa ameshawaza kuja kuwa diwani, kampuni yangu tukishirikiana na ya moja ya South africa tulikosa, na tulijua tumekosa mda mrefu sana.

Siyo mradi wa Ukawa wala CCM, ni wa World Bank, hivyo meya kaamua kuubeba juu juu kisiasa, kama kweli tunataka maendeleo tuacheni hizi mbwembwe jamani, hazifai si kwa CCM wala UKAWA, imetosha sasa tuhudumieni wananchi
 
Back
Top Bottom