pwilo
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 11,585
- 14,669
Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania na EID njema kwa waislamu wote na watanzania wote tuliobahatika kuiona siku ya leo.
Leo nataka niongee na ndugu zangu waliojiriwa katika sehemu mbalimbali nchini kwetu maana hakuna watu wanapitia kipindi kigumu kama watumishi na wafanyakazi wengine waliojariwa kwasababu kikawaida mishahara huwa inatoka tarehe 22 mpaka tarehe 25 kila mwezi.
Ikumbukwe mwezi huu ulikuwa na sikukuu mbili ilianza ile ya PASAKA kwa ndugu zetu wa kristo halafu ikafuatiwa na EID ELFITIR kwa waislamu na kama unavyojua kipindi cha sikukuu matumizi yanakuwa makubwa sana hvyo kufanya wafanyakazi kuwa na kipindi kigumu sana mtaani na kula msoto mkubwa kutokana na sikukuu mbili kugongana kwa pamoja.
Labda niwakumbushe tu watumishi na wafanyakazi wote hayo maisha na msoto mnaopitia sasa hivi ndio maisha mtakayoishi baada ya kustaafu kwa hyo akili kichwani mwenu ila inakuaje mtu anafanya kazi miaka 10 lakini mshahara ukichelewa siku mbili tu wanaanza kulalamika inakuwaje hili wazee maana mshahara wa mwezi umeisha kabla haujatoka kwa madeni waliyonayo watumishi.
Kiufupi hichi kipindi ndio cha kujiandaa na kutafakari maisha yako kabla ya kustaafu maana watumishi mnajisahau sana ila inakuaje SERIKALI inashindwa kuwapa wafanyakazi wake angalau mkono wa sikukuu na badala yake wananunua magoli ya simba na yanga million 10 hivi nani alituroga watanzania tupo kama mazuzu vile.
Pesa zenu za NHIF,NSSF zinachotwa mpo tu zile ndio mlitakiwa muwe na uwezo wa kukopa kipindi kama hichi bila riba ili ziwasaidie ila wengine wanachota bila uoga halafu wahusika mnabaki tu kuishi maisha ya taabu na kulalamika na kusubiria siku ya mei mosi kupewa kofia na T shirt.
Poleni watumishi na wafanyakazi wote kwa msoto mnaopitia nyinyi na watu muhimu sana kwenye taifa letu siku mkijatumbua.
Alamsik na EID njema from my family to yours.