‘Msizungumze maneno yasiyo na tija kwa taifa’

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Damian Lubuva amewataka wanasiasa walioshindwa katika uchaguzi mkuu uliopita wajipange kwa ajili ya uchaguzi ujao wa mwaka 2020 na si kuzungumza maneno ambayo hayana tija kwa taifa.

Alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati akifungua mkutano wa tathimini wa asasi za kiraia kuhusu elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

“Uchaguzi umekwisha wanasiasa msiwapotoshe wananchi, walioshinda wameshinda na walioshindwa wameshindwa sasa tujipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020… wanaotoa hukumu kwenye uchaguzi ni wananchi wenyewe sio Tume wananchi kwa utashi wao huchagua wanayemtaka,” alisema.

Alisema katika uchaguzi mkuu uliopita Tume ya Uchaguzi haikuwa na chama wala haikupendelea chama chochote bali ilifanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za nchi na kuongeza kuwa hakuna hata mgombea mmoja aliyekwenda tume kuonesha ushahidi kuwa aliibiwa kura.

Jaji Lubuva alisema kumekuwa na maneno kuwa tume inatakiwa ifukuzwe kutokana na kuonekana kukipendelea chama fulani.

Akitoa mfano alisema mwaka 2010 watu milioni 20 walijitokeza kujiandikisha lakini waliopiga kura ni milioni nane na pia mwaka 2015 jumla ya watu waliojiandikisha walikuwa milioni 22.5 lakini waliopiga kura ni milioni 15.5.

Jaji Lubuva alisema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kura zilizoharibika zilikuwa 227,889 sawa na asilimia 2.65 wakati katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 kura zilizoharibika zilikuwa ni 402,248 sawa na asilimia 2.5, hali ambayo inaonesha watu wakielimishwa kura zinazoharibika zinapungua.

Mwenyekiti huyo wa tume alisema mwaka 2015 jumla ya asasi za kiraia zilizoomba kutoa elimu ya mpiga kura zilikuwa 551 lakini asasi zilizoruhusiwa kufanya hivyo zilikuwa 447.
 
Hili nalo neno,manake kuna aliyekuwa mgombea "mashuhuri"mpaka leo analia lia kwamba alipokwa ushindi.Porojo za namna hii ni za kukemewa kwa nguvu.
 
Umenena vema Jaji Lubuva. Sasa hao walioshindwa wanaposema kuwa walishindwa kwa sababu matokeo yalichakachuliwa(na tume), kwanini usiwachukulie hatua za kisheria ili wathibitishe madai yao? Na wakishindwa hatua stahiki zichukuliwe. Kuwaacha waseme tu kunawafanya wengine wawaamini na kuweka uchungu mioyoni mwao dhidi ya aliyeshinda, chama na serikali iliyoko madarakani, wapenzi wa chama kilichoshinda na pia tume iliyosimamia uchaguzi. Hii ni hatari kwa amani wa taifa letu. Natoa rai kwako wanasiasa hawa uchwara wanapotuhumu tume kwa uchakachuaji wa kura usiwachekee na usijitetee magazetini, wafikishe mahakamani sheria ichukue mkondo wake.
 
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Damian Lubuva amewataka wanasiasa walioshindwa katika uchaguzi mkuu uliopita wajipange kwa ajili ya uchaguzi ujao wa mwaka 2020 na si kuzungumza maneno ambayo hayana tija kwa taifa.

Alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati akifungua mkutano wa tathimini wa asasi za kiraia kuhusu elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

“Uchaguzi umekwisha wanasiasa msiwapotoshe wananchi, walioshinda wameshinda na walioshindwa wameshindwa sasa tujipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020… wanaotoa hukumu kwenye uchaguzi ni wananchi wenyewe sio Tume wananchi kwa utashi wao huchagua wanayemtaka,” alisema.

Alisema katika uchaguzi mkuu uliopita Tume ya Uchaguzi haikuwa na chama wala haikupendelea chama chochote bali ilifanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za nchi na kuongeza kuwa hakuna hata mgombea mmoja aliyekwenda tume kuonesha ushahidi kuwa aliibiwa kura.

Jaji Lubuva alisema kumekuwa na maneno kuwa tume inatakiwa ifukuzwe kutokana na kuonekana kukipendelea chama fulani.

Akitoa mfano alisema mwaka 2010 watu milioni 20 walijitokeza kujiandikisha lakini waliopiga kura ni milioni nane na pia mwaka 2015 jumla ya watu waliojiandikisha walikuwa milioni 22.5 lakini waliopiga kura ni milioni 15.5.

Jaji Lubuva alisema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kura zilizoharibika zilikuwa 227,889 sawa na asilimia 2.65 wakati katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 kura zilizoharibika zilikuwa ni 402,248 sawa na asilimia 2.5, hali ambayo inaonesha watu wakielimishwa kura zinazoharibika zinapungua.

Mwenyekiti huyo wa tume alisema mwaka 2015 jumla ya asasi za kiraia zilizoomba kutoa elimu ya mpiga kura zilikuwa 551 lakini asasi zilizoruhusiwa kufanya hivyo zilikuwa 447.
kama yeye ni mkweli azungumzie suala la umeya dar kwa nini mpaka leo hii meya hajapatikana? hayo ndio masuala ya siasa, umeya kwanza
 
Bado kuna watu hawajatangaza kumtambua magufuli
Wamtambue wasimtambue yeye ndiyo Rais, na kutokumtambua kwao hakumzui yeye kutimiza majukumu yake.Hawmtambui na wakati sasa hivi wengine wako kwenye kamati kujadili bajeti iliyoandaliwa na serikali yake hahahahahaa hawa jamaa ni zaidi ya wasanii.
 
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Damian Lubuva amewataka wanasiasa walioshindwa katika uchaguzi mkuu uliopita wajipange kwa ajili ya uchaguzi ujao wa mwaka 2020 na si kuzungumza maneno ambayo hayana tija kwa taifa.

Alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati akifungua mkutano wa tathimini wa asasi za kiraia kuhusu elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

“Uchaguzi umekwisha wanasiasa msiwapotoshe wananchi, walioshinda wameshinda na walioshindwa wameshindwa sasa tujipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020… wanaotoa hukumu kwenye uchaguzi ni wananchi wenyewe sio Tume wananchi kwa utashi wao huchagua wanayemtaka,” alisema.

Alisema katika uchaguzi mkuu uliopita Tume ya Uchaguzi haikuwa na chama wala haikupendelea chama chochote bali ilifanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za nchi na kuongeza kuwa hakuna hata mgombea mmoja aliyekwenda tume kuonesha ushahidi kuwa aliibiwa kura.

Jaji Lubuva alisema kumekuwa na maneno kuwa tume inatakiwa ifukuzwe kutokana na kuonekana kukipendelea chama fulani.

Akitoa mfano alisema mwaka 2010 watu milioni 20 walijitokeza kujiandikisha lakini waliopiga kura ni milioni nane na pia mwaka 2015 jumla ya watu waliojiandikisha walikuwa milioni 22.5 lakini waliopiga kura ni milioni 15.5.

Jaji Lubuva alisema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kura zilizoharibika zilikuwa 227,889 sawa na asilimia 2.65 wakati katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 kura zilizoharibika zilikuwa ni 402,248 sawa na asilimia 2.5, hali ambayo inaonesha watu wakielimishwa kura zinazoharibika zinapungua.

Mwenyekiti huyo wa tume alisema mwaka 2015 jumla ya asasi za kiraia zilizoomba kutoa elimu ya mpiga kura zilikuwa 551 lakini asasi zilizoruhusiwa kufanya hivyo zilikuwa 447.
Kama wanavunja sheria wawashtaki. Otherwise let them talk. Wewe umeshinda inakuuma nini mtu akisema ameshinda wakati medali unayo wewe.

Utakuwa mjinga usipoangali which side of your bread is buttered. Tusilaumu sana taasisi.
 
Wamtambue wasimtambue yeye ndiyo Rais, na kutokumtambua kwao hakumzui yeye kutimiza majukumu yake.Hawmtambui na wakati sasa hivi wengine wako kwenye kamati kujadili bajeti iliyoandaliwa na serikali yake hahahahahaa hawa jamaa ni zaidi ya wasanii.
Mkuu hao wote NJAA KALI watu wa pwani husema WANAJISHAUA TU.
Ooh eti hatumtambui mbona akitoa amri wanaufyata
 
Back
Top Bottom