kamati ya ufundi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 416
- 439
MSISIMKO WA UWEKEZAJI NA VODACOM TANZANIA.
Baada ya kuwa wa kwanza katika kujiandikisha katika soko la hisa Kampuni ya Vodocom, Imetoa nafasi kwa wananchi wa kawaida kuweza kumiliki kampuni hii ambayo imekuwa ikitengeneza faida ‘nono’ kila mwaka.
Wananchi walionunua hisa Vodocom Tanzania wanaingia kwenye kampuni kubwa zaidi katika soko la huduma za mawasiliano kwa simu za kiganjani kati ya kampuni saba, Vodacom inachukua asilimia 31 ya soko na laini milioni 12.06 hadi kufikia Juni mwaka huu.
Kampuni za Tigo na Airtel zinashikilia nafasi ya pili na ya tatu kwa kuwa na asilimia 29 na 26 ya soko. Kampuni ya Tigo ina laini milioni 11.6, huku kampuni ya Airtel ikiwa na laini milioni 10.3.
kwa miaka zaidi ya 17, Kampuni ya simu ya Vodacom imekuwa kinara katika ulipaji kodi kutokana na mwenendo wa kibiashara kwa kampuni hiyo sasa kutaweka wazi hali ya utendaji na mwenendo wa kampuni hiyo
Tangu kuingia sokoni tarehe 17 mwezi wa tatu watu wengi wamekuwa wakizifuatilia hisa za Vodacom kupitia nakala ya matarajio yake inaonyesha financial statements yao ya mwaka 2016 na projections ya 2017 na 2018 ni zakuvutia sana kulinganisha na kampuni nyingine zinazofana na Vodacom.
Ukitazama katika Annual revenue yao ni kubwa kuanzia bilioni 900 mpaka 1 Trilioni
kwa kwa kipindi cha maombi hadi siku ya leo ambapo imebaki siku moja kufungwa kwa maombi ya hisa upo uwezekano wa bei kupanda juu mara baada ya kufungwa kwa maombi ya hisa za Awali ikitegemewa na hali ya uchumi wa nchi.
Ukitizama sera yao ya gawio imewekwa wazi kabisa baada ya Faida ya asilimia 50 baada ya makato ya kodi kwa mwaka na Gawio litakwenda kwa kila mwanahisa wa kampuni.
Kwa rational investors wakifanya mahesabu wanaweza kuona kwamba Uwekezaji kwenye Vodacom ni chaguo bora kwa current financials na projections ya 2017 na 2018.
Hatua ya makampuni ya simu kujiorodhesha DSE ni utekelezaji wa sheria ya Elektroniki na Mawasiliano ya Posta (EPOCA) na Sheria ya Fedha ya mwaka 2016 inayoelekeza makampuni ya simu kumilikishwa asilimia 25 ya hisa zake kwa wananchi.