Miaka kadhaa iliyopita Kibaki alitaka kufanya hichi anachokifanya sasa Jakaya ya kuandika katiba anayoitaka yeye sasa baadae kutakiwa kuwa na kura ya maoni kuikubali au kukataa njia hii.Wapenda mageuzi wa kweli wakajipanga na kupita nchi nzima kuipinga na kuwashawishi watu waikatae kwa kupiga 'NO' walijulikana kama orange,na upande wa Kibaki wa 'YES' ulijulikana kama ndizi.
Upande wa 'NO' au Orange ulishinda na hivyo kumlazimisha Kibaki kutumia njia ya kuwashirikisha Wakenya wote katika kuandika na kupitisha Katiba hii nzuri waliyoipata sasa.
Kwahiyo ni kujipanga tu wakati wa kura ya maoni kuhamasisha wananchi kuikataa Katiba hii,inawezekana kila mmoja akishiriki kikamilifu.
Mkuu' muswaada unasema kama kura za hapa zitashinda' basi katiba iliyopo itaendelea.
mimi mwenyewe sikubali kura ipigwe na kama ikipigwa isimamiwe na nani? Mbona imezoeleka kila siku tunachagua nyekundu tunaletewa kijaniMkuu uporoto kuna kitu nataka ujue,tukikosea step tukakubali kura ipigwe tumekwisha lazima watashinda,hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindanna na ccm tunapoongea mambo ya kura,ni wazoefu wa kuchakachua,hilo siafiki hata kidogo
nimeipenda hii, saluti mkuu!Mchakato huu hauna tofauti na mbuni aliyeficha kichwa chake shimoni hali mwili wote uko nje. Bunge limetumika kupitisha uozo mwingi sana wa serikali ya CCM, matokeo yake tunayajua. Hatujakoma tunazidi kufanya madudu yaleyale, na matokeo yatakuwa yaleyale. Mchakato mbovu, utazaa kamati mbovu, itakayokusanya maoni na kurudisha ripoti mbovu, itapelekwa kwenye bunge la katiba bovu, lenye idadi kubwa ya wawakilishi walioanzisha mchakato mbovu, watapitisha rasimu ya katiba mbovu, kwenda kupigiwa kura ya maoni itakayosimamiwa na tume mbovu. KATIBA ITAKUWA MBOVU
Mkuu uporoto kuna kitu nataka ujue,tukikosea step tukakubali kura ipigwe tumekwisha lazima watashinda,hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindanna na ccm tunapoongea mambo ya kura,ni wazoefu wa kuchakachua,hilo siafiki hata kidogo