msingi wa katiba mpya

MWITA BUGONGO

Member
Joined
Jun 5, 2014
Posts
19
Reaction score
8

Msingi wa Katiba Mpya

Kuanza kwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba kuna historia inayotokana na kumbukumbu ya michakato mitatu iliyokwama, Harakati hizo zilianza kujitokeza tangu mwaka 1992 kupitia Tume ya marehemu Jaji Francis Nyalali.Tume hiyo ilikuwa chini ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.

Sehemu ya mapendekezo ya tume hiyo, ni mapendekezo ya kufanya mabadilko makubwa katika Katiba ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini hata hivyo mapendekezo hayo yaligonga mwamba na badala yake ikawekewa viraka vya mfumo mpya wa vyama vya siasa.

Baada ya hapo, tukawa na Tume ya Jaji Robert Kisanga (White paper), mwaka 1998. Nayo ilifanikiwa kukusanya mapendekezo kadhaa ikiwamo yaliyolenga kuboresha muundo wa serikali, lakini hata hivyo yalitupiliwa mbali.

Kabla ya hiyo, mchakato mwingine ulikuwa ni mapendekezo ya umoja wa wabunge kutoka upande wa Bara la G55, mwaka 1986 yaliyokuja na mapendekezo ya kudai uwepo wa Serikali ya Tanganyika lakini hata hivyo pia yalitupiliwa mbali.

Kutokana na mazingira hayo, Mkurugenzi wa taasisi ya kufuatilia mwenendo wa shughuli za Bunge (CPW), Marcossy Albanie anasema kinachoendelea kufanyika ndani ya utawala wa CCM ni majaribio ya kupima imani ya Watanzania kama watakuwa tayari wamebadilisha msimamo wao juu ya serikali tatu.

“Tangu mwaka 1986, Tume zilikuwa zinapendekeza serikali tatu, wanachokihofia CCM ni kwamba, endapo watakubaliana tu na mapendekezo hayo, basi huo ndiyo utakuwa mwisho wa utawala wao Zanzibar, hiyo ndiyo siri kubwa inayoiumiza kichwa CCM,” anasema Albanie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…