MSIMU HUU WENGER AKILEGEA HAINGII TOP FOUR

FATHER OF REALITY

Senior Member
Nov 3, 2014
122
99
Niliwahi kusema hili katika post yangu titled "makocha wazawawa uingereza wanadumaza soka la nchi yao". Nilipata hofu kubwa juu ya mpira wa mazoea wa waingereza hasa kwa timu kama Arsernal kufikiri kwamba top four ni eneo maalum ambalo timu hiyo haikosekani, nilitishwa na uwepo wa Jose Mourinho Man U, Pep City, Potchetino Spurs, Antonio Conte Chelsea, Klop Liver na hata bingwa mtetezi Raniel ambaye ameonekana kusua sua katika ligi kuu England msimu huu, NILICHOKIJUA KWA WALIMU HAWA NI KWAMBA WABISHI KIUFUNDI PIA WASHINDANI WA MAFANIKIO, NIKAPATA SHAKA.

Niliandika vile nikimaanisha kutokana na technical know how ya hawa walimu wapya ambayo ipo mbali sana na waalimu wa asili ya kiingereza au hata walioanzia kufundisha soka chini humo. Ni kwa muda mrefu sana wenger na ferguson walisumbua soka ya nchi hii huku wakati mwingine viwango vya wote vikiwa vya kusa sua ukilinganisha na timu kubwa kama hizo nje ya uingereza, ni takribani miaka nane sasa timu kongwe ya Arsenal imekuwa ikitembea katika mwendo mpya uliobadili kabisa hata hisia za mashabiki kutoka kujiamini hadi kutojiamini kama timu nyingine imara na hasa mbele ya hao waitwao wakubwa wenzao.

Lakini cha kushangaza pamoja na wengi kudai ligi hiyo ina ushindani mkubwa kisoka, jambo ambalo si la kubeza, bado hawa Arsernal ambao mvuto na umahili wao wa kutawala soka umepotea kwa kiwango kikubwa, hawajawahi maliza ligi nje ya nne bora (top four), kweli tumeona timu kama Barcelona, Madrid na Bayern zikiwa ndani ya top four zaidi ya miaka 12, lakini huonyesha kiwango kinachoshawishi kwamba wanastahili kuwa hiyo top four. pindi timu hizo zinapotetereka kiviwango, huwa zinapotea hata hiyo top five. Mfano Real madrid ilishika nafasi ya 6, 5 2000 na kurudi nyuma, barcelona ya 5,6,na hata ya 8 nyuma ya 2000.

Naamini kwamba jambo hilo la kuporomoka kwa asernal toka nafasi ya nne halijatokea si kwa sababu Arsernal ni bora sana la hasha, bali ni udhaifu wa viwango vya timu pinzani za Uingereza ambazo hazina ushindani hasa wa kiufundi hivyo wamemzoeza wenger kushikilia nafasi na kuifanya timu yake ionekane moja ya timu bora huko ulaya, lakini siri hufichuka pale wanapoelekea klabu bingwa ulaya tunapokuta Arsernal inasumbuliwa hata kwa magoli ya taabu au hata kusuluhu na zile timu zipigwazo mara kwa mara magoli 8 au 7, au 6 au 5 au zimebahatika goli 4 na timu babe kama Barca. Madrid, Atletico, Juve, Bayern, Milan (wote katika ubora).

Na hakika haya maneno yatatimia kwa maana wale wabishi mithili ya Ferguson na Jose wamekuwa wengi, nilitamani sana kocha kama Anceloti, Mancini na Pelegrini wangekuwepo kuongeza idadi ya wabishi na mafundi. Wenger alikuwa kocha mzuri sana lakini waingreza namna ya uchezajiwao na ufundi wao uliofinyu, umemdumaza, kwa sasa anapokutana na timu kama Barcelona, Bayern na zinginezo anaenda kama timu ndogo ndogo akitarjia kutolewa mashindanoni kuliko kubaki.

jambo hili nimelitolea mafno kwa Arsernal si kwamba wengine wapo salama, yaani ni hivi ukikutanisha timu ya Ujerumani, au Itali au Hispania na ukaambiwa mwaka huo za uingereza zipo kwenye ubora na hizo nyingine pia zipo kwenye ubora, timu za uingereza uwa hazishindi confortably, uwa zinacheza na mashaka makubwa kana kwamba zimejiandaa kutolewa, uwa zinakubali baadhi ya mambo kirahisi kama vile kuchezewa sana mpira huku zikisubili kupata magoli ya kuvizia na mara nyingi zimekuwa zikitupwa nje.

tumeona ubabe wa akina totenham, Man city, EVERTON, LIVERPOOL, Southampton n.k zinapodhairirishwa kirahisi huko nje na hata timu za EUROPA.

NB: MAKOCHA WOTE WALOLETA MAFANIKIO MAKUBWA VILABU VYA UINGEREZA ASILIMIA 98% SI WAINGEREZA.
 
Back
Top Bottom