Msimbazi si shwari

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,843
Reaction score
10,768
Nimepita mitaa ya msimbazi na kukuta makundi makubwa ya wapenzi na wanachama wa Simba wakirusha maneno ya shutuma dhidi ya viongozi waliofanya mapinduzi. Kilichonishitua zaidi ni pale walipokuwa wakijadili uwezekano wa kuchoma moto gari la Kaburu (Nyange?). Kwamba ndiye chanzo cha yote. Pia kuna shutuma kuwa akins mzee wa Kinesi ni mapandikizi ya Yanga.

Mtazamo wangu: Rage anaufuasi mkubwa sana klabuni ni si rahisi hata kidogo kumwondoa. Kwa mujibu wa radio moja ya jijini, Rage amedai kuwa mwenye mamlaka ya kuitisha kikao cha kamati ya utendaji kikatiba ni mwenyekiti au makamu wake. Tatizo ni kuwa Simba mpaka sasa haina makamu mwenyekiti kwani aliyepo anakaimu tu, hivyo kukifanya kikao kilichoitishwa kuwa cha kitchen party. Ngoma inogile.
 
Hiyo ndege si ianguke tu huyu jamaa asirudi ananikera. Yan wapenzi wa simba tumekuwa wanyonge kwa sababu yake
 
Kikao cha Kitchen Party kimemsimamisha Mwenyekiti wa Timu ya Mpira wa Miguu mbona haiwezekani, bora hata kikao cha harusi kina wanaume wengi zaidi.
 
...kama ndo hivyo hii timu isiitwe tena Simba Sports Club(SSC) badala yake ipewe jina la Rage Sports Club(RSC).
 
Siku yanga na simba zikifa ndo mpira wetu utakua.there is nn way soka letu likaendlea kama yanga na simba zenye watu kama mzee akilimali na rage zitakua hai.
 
Soka linazidi kudidimia kwa minajili ya m2 mmoja, cjui achapwe viboko kwanza ndo ajue wenye cmba wapo!
 
popote nisikiapo neno Rage nashikwa na hasira sana,na mishabiki ya simba imezidi kuwa mipopompo,ona yanapinga kusimamishwa Rage,kudadeki zenu bora mshuke daraja kabisa...aaaaaarghhh
 
Me niliwashangaa sana Simba, hivi walikosa mtu wa kuwa Mwenyekiti wakaamua kumchagua Msomali tena mbaya zaidi mwanaCCM? Majanga!!!!!
 
Hii vita bora rage ashinde tu ili simba iendelee kufanya vibaya na hatimaye ishuke daraja.
 
me niliwashangaa sana simba, hivi walikosa mtu wa kuwa mwenyekiti wakaamua kumchagua msomali tena mbaya zaidi mwanaccm? Majanga!!!!!

matusi hayo sasa kwahiyo kuwa mwana cmm nikosa,hakili za kushikiwa mbaya sana unaonekana mtu mzima mwenye busara kumbe punga dizine
 
matusi hayo sasa kwahiyo kuwa mwana cmm nikosa,hakili za kushikiwa mbaya sana unaonekana mtu mzima mwenye busara kumbe punga dizine
Ngumu sana kuielewa post yako mkuu, hebu jipange uandike upya au mwite mwenzio akusaidie kuedit na kupost!!!
 
matusi hayo sasa kwahiyo kuwa mwana cmm nikosa,hakili za kushikiwa mbaya sana unaonekana mtu mzima mwenye busara kumbe punga dizine

duu sasa hapo nani mwenye busara kati yenu?
 
popote nisikiapo neno Rage nashikwa na hasira sana,na mishabiki ya simba imezidi kuwa mipopompo,ona yanapinga kusimamishwa Rage,kudadeki zenu bora mshuke daraja kabisa...aaaaaarghhh
....inashangaza sana kwakweli; RAGE anaongoza Club utafikili anaongoza familia yake(mke na watoto wake) kwa upuuzi wote anaoufanya alafu jamaa wanaojiita wakereketwa wanaendelea kumkumbatia. Inatia hasira kwakweli.
 
Hiyo ndege si ianguke tu huyu jamaa asirudi ananikera. Yan wapenzi wa simba tumekuwa wanyonge kwa sababu yake
Una hakika hao abiria wengine wote kwenye hiyo ndege ni wanachama wenu wanaomuunga mkono Rage? Yaani uuwe watu wote hao kwa sababu ya kosa lenu wenyewe la kumchagua mtu mnayemwogopa kumwondoa kikatiba?
 
Nawaomba sana tena sana watani yanga pelekeni kipigo cha magoli ya uhakika pale msimbazi, ili kenge atokwe damu masikioni atatambua kumbe napigwa eeh!

kwa sasa naishabikia mbeya city.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…