gwamaka aswile
Senior Member
- Mar 26, 2015
- 186
- 106
MSIMAMO WA SUMAYE KISIASA NI WA KIITIKADI AU KIMASLAHI?
Na. Gwamaka Aswile
Neno siasa lina tafsiri nyingi. Frank Underwood, muigizaji mkuu wa tamthiliya ya kwenye runinga ya ‘House of Cards’ aliwahi kutafsiri mchakato wa kusaka madaraka kwa maneno haya: “Njia ya kusaka ama kuelekea kwenye madaraka imepambwa/ imesakafiwa na unafiki na majeruhi”
Bill Clinton, rais wa zamani wa Marekani aliwahi naye kutoa tafsiri ya neno siasa katika hotuba yake aliyoitoa kwenye kongamano na wanafunzi mnamo July 13, 2005, alisema: “Siasa ni hangaiko la mahitaji linalofichwa katika ushindani wa kanuni na misimamo. Ni namna ya kufanya mambo ya umma kwa maslahi binafsi”
Naye mwanafasihi wa Kiingereza K.J. PARKER anasema kuwa katika siasa mambo ambayo hayazungumzwi wazi ndiyo ambayo ya kuangaliwa zaidi. “In politics, it's what isn't said that matters.” Kwa maana nyingine maneno wanayosema wanasiasa na dhamira zao ni vitu viwili tofauti.
Hivi karibuni aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tatu, Fredrick Tluway Sumaye alitangaza kukihama Chama Cha Mapinduzi(CCM) na kukimbilia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKWAWA) ambako alijiunga na UKAWA.
Akiongea katika Hoteli ya Ledger Bahari Beach jijini Dar es Salaam aliporomosha tuhuma dhidi ya CCM, aliyoitumikia tangu mwaka 1983 alipogombea ubunge wa Hanang na kushinda kuwa haijali demokrasia.
Katika maelezo yake, Sumaye ambaye pia miaka ya nyuma aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Ushirika kuanzia mwaka 1985 hadi 1994, alisema ameamua kuhama chama hicho baada ya kuchoshwa na ukandamizaji wa demokrasia ndani ya CCM.
Kwa mtu anayeifahamu vyema historia ya Sumaye ambaye alidumu kwa muda wa miaka kumi madarakani kuanzia mwaka 1995 hadi 2005, atagundua kwamba lipo jambo kubwa lililojificha nyuma ya kauli zake.
Sumaye amekuwa ni mtu ambaye ameonesha nia ya kuutaka Urais wa Tanzania kwa muda mrefu. Inawezekana baada ya kuhudumu katika cheo cha Uwaziri Mkuu wakati wa utawala wa Rais Mkapa tangu mwaka 1995 hadi 2005, akili yake ilimuambia na kumuaminisha kuwa anao uwezo wa kushika nafasi ya juu zaidi.
Sumaye ambaye aliwahi kushika nafasi ya juu kabisa ya kiuongozi ya Uwaziri Mkuu, alikuwa na nafasi ya kuweza kufanya mambo ambayo yangeweza kuibadilisha Tanzania kutoka hapa ilipo na pengine tungekuwa na nchi ambayo inayo Maendeleo makubwa kupita haya. Yeye hakuweza kufanya hayo aliyoyasema.
Sumaye ambaye alishindwa kuibadili Tanzania na kuwa nchi bora zaidi kama alivyosema wakati akichukua fomu za kutaka kugombea Urais kupitia CCM, anaamini kabisa kuwa kwa kwenda kwake UKAWA ataweza kutoa miongozo ambayo itawaimarisha na kuwafanya imara tayari kwa kuongoza nchi.
Kumfahamu vizuri Sumaye yafaa tuiangalie kwanza historia ya nchi kwa ujumla. Kwanza, tangu tupate uhuru tushawahi kuwa na mawaziri wakuu wafuatao: Julius Kambarage Nyerere, Rashid Kawawa, Edward Moringe Sokoine, Salim Ahmed Salim, Joseph Sinde Warioba, John Malecela, Cleopa David Msuya, Edward Ngoyai Lowassa na Mizengo Pinda.
Ni wazi kuwa si vibaya kwa mtu ambaye alishawahi kushika nafasi ya Uwaziri Mkuu kugombea apitishwe kwenye nafasi ya Urais. Aliwahi kufanya hivyo Cleopa Msuya, John Malecela, Salim Ahmed Salim, pia amefanya hivyo Mizengo Pinda na Sumaye. Ni haki ya kikatiba na ya msingi kwa mtu yeyote kufanya maamuzi hayo.
Kwa maana hiyo, haikuwa ajabu pale mwaka 2005, baada ya Mkapa kumaliza muda wake, Sumaye ambaye alikuwa ni Waziri Mkuu wake kuwa ni miongoni mwa watangaza nia ambao walionesha kiu ya kutaka kupitishwa kuwa wagombea Urais na hivyo, kupata wasaa wa kuitumikia nchi.
Sumaye alikwenda mbali katika kinyang’anyiro hicho na kuingia kwenye hatua ya tano bora lakini baada ya mchujo wa kura, Kikwete ndiye aliyepita na kugombea Urais kupitia CCM. Yapo maneno kuwa katika mchakato huo, chaguo la Rais Benjamin Mkapa lilikuwa ni Sumaye na Lowassa alikuwa pamoja na Kikwete.
Sumaye hakuridhika sana na kushindwa kwake ingawa alikubaliana na maamuzi. Aliendelea na harakati zake za kutaka cheo cha juu na katika kujiongeza kimaarifa, mwaka 2006 alikwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Havard katika Shule ya Uongozi ya John F. Kennedy ambako alihitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Umma.
Mwaka 2012, waziri mkuu huyu mstaafu alishiriki tena kwenye uchaguzi wa ndani ya chama chake hata hivyo akiwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) wilayani Hanang. Hata hivyo, Sumaye alishidwa katika kinyang’anyiro hicho, akiangushwa na Dk. Mary Nagu. Sumaye alipata kura 481 huku Dk. Nagu akiibuka na kura 648.
Baada ya kushindwa Sumaye aliongea. Alisema kuwa kushindwa kwake huko kulichangiwa na matumizi makubwa ya fedha ambazo zilitolewa na wapinzani wake waliomuona kuwa anaweza kuharibu ndoto zao za kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2015. Hakutaja jina ila watu waliofuatilia hali ya kisiasa walijua kuwa alikuwa anamlenga nani.
Siku zikapita na hatimaye ukaja mchakato wa kutafuta mgombea Urais kwa tiketi ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi wa mwaka 2015. Kama watia nia wengine Sumaye naye alijitokeza na kutangaza nia yake ya kutaka kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi.
Wakati akitangaza nia alisikika akisema kuwa iwapo CCM itampitisha mtu ambaye ana tuhuma za ufisadi yeye hatomuunga mkono na yupo tayari kuhama chama. Yapo madai kuwa hata akiwa kwenye vikao vya ndani alikuwa akisikika akiyaongea maneno hayo mara kwa mara. Ulipofika wakati wa maamuzi matokeo yalipotoka kati ya majina ya makada 38 waliorudisha fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea Urais ni matano tu ndiyo yaliyokuwa yamerudi.
Baada ya mchakato wa kura ndipo jina la John Pombe Magufuli likaibuka kidedea. Mambo mengi yametokea baada ya mchakato wa CCM. Tumeshuhudia watu wakihama vyama, viongozi wakubwa wa chama wakitangaza kuhama nafasi zao na maamuzi mengine ya aina hiyo.
Hata hivyo, uamuzi uliochukuliwa na Sumaye umezua gumzo. Kwa mtu yeyote anafanya tafakuri, ni ngumu sana kumpima waziri mkuu huyu mstaafu katika mizania ya kikanuni na kiitikadi. Haiwezekani kujua dhamira halisi ya mtu huyu ni nini?
Mara nyingi amekuwa ni mtu anayekaa kimya ila hupenda kuibuka nyakati za vinyang’anyiro mbalimbali ndani ya chama na anapokosa nafasi hutoa maneno mazito. Mara zote akikosoa maamuzi yaliyofanywa kwa kuzingatia vikao na kanuni.
Swali hapa ni je, iwapo angepitishwa yeye kuwa mgombea angeongea maneno hayo hayo? Unaposema kuwa wapinzani hawajakomaa kwenye masuala ya kiutawala unakuwa unamaanisha nini? Sumaye ambaye wakati wake aliwahi kutetea matumizi ya takrima kuwa ni jambo zuri tu la kiungwana. Baadaye alipozongwa na vyombo vya habari akabadili maneno ni mtu wa kuaminika kwa kiasi gani?
Kwa mtazamo wa haraka inaonekana Sumaye ni mtu ambaye anataka madaraka ya juu kabisa ya nchi. Ni mtu ambaye anataka Urais sasa ameona kuwa malengo na matumaini yake hayajafikiwa ndipo ameamua kuhama chama. wasiwasi wangu ni kuwa hata kama CCM wangempitisha Lowassa upo uwezekano wa Sumaye angeitisha tena mkutano wa vyombo vya habari na kutangaza kuhama chama na sababu ambayo angeweza kuitoa ni kuwa CCM inakumbatia wala rushwa na kwamba yeye hawezi kukaa chama kimoja na wala rushwa.
Ni hapa sasa ndipo ninapoyaamini maneno ya Frank Underwood, kuwa “Njia ya kusaka ama kuelekea kwenye madaraka imepambwa/ imesakafiwa na unafiki na majeruhi” Ni juu yetu wananchi kutafakari mienendo ya viongozi wetu kama ni kutuangalia sisi wananchi au ya kujiangalia wao binafsi.