Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
Nashindwa kuelewa, kitu hapa.
TBC waliamua kusitisha kurusha live bunge na kuanza kurikodi.
Jambo hili lilipingwa na walipa kodi
Hata hivyo ikatokea taasisi ya kuisadia TBC kwa kulipa gharama za urushaji
Pia Azam na Star TV wao walikuwa na mpango wa kuendelea kurusha live.
Star TV wakitumia channel yao ya bunge katika kisimbusi chao cha Continental
Azam wao walikuwa wanatumia Azam Two, Azam One na Au Azam Extra
Kwa hivyo tulitaraji bunge la bajeti kurushwa live, aidha na TBC baada kufidiwa, au kwa vituo binafsi.
Baada ya Nape Moses Nnauye kuona hilo na huku akishikilia msimamo wake uleule alo kuwa nao kabla ya kuwa mbunge na waziri, msimamo wa bunge wa kutorushwa live, hatimaye bunge sasa likaanzisha studio zake na vyombo vyote binafsi na pamoja na TBC kutakiwa kufungua na kutofunga camera na mitambo yao katika ukumbi wa bunge.
Studio za bunge zilisema wao ndio watachukua na kurusha matangazo hayo, kisha vyombo vinavyo hitaji vitayachukua na kusambaza kwa walaji.
Matarajio yetu kama walaji na walipa kodi na wenye haki ya kufuatilia bunge ni studio za bunge kurusha kila jambo na kila tukio linaloendelea katika ukumbi wa bunge hapo kwa papo(live) ili TBC iliyopewa fedha za kurusha live wapate, lakini pia na vyombo vingene vipate.
La kusikitisha, studio za bunge zinarusha live matangazo ya maswali na majibu tu, lakini mijadala mingine yote itarekodiwa na watarusha kwa muda ambao wenyewe wamepanga na kwa muda huo ndio vyombo vingine vitapata.
Yaani, hata kama AZAM au STAR TV wataka kurusha live, lakini watashindwa kufanya hivyo midhali Nape hataki bunge lionekane live, Hili ni lake Nape tangu mwaka 2013, sema alishindwa kulitekeleza sababu hakuwa katika mamlaka.Kwa hili nashawishika kumchukia Nape na rais Magufuli. Hawatutendei haki na hoja zao hazina mashiko.
Sababu kuu mwanzo ni kuwa TBC haina fedha, lakini sasa fedha imeihidiwa kupewa, Azam na Star Tv wako tayari kurusha na wao walisema lile Tangazo lilikuwa kwa TBC tu na ya kwamba vyombo binafsi vinaweza kuendelea na utaratibu wao, mbio za sakafuni huishia ukingoni, Nape kafika ukiongoni, kwa kujua hilo ndio kaja na hili la studio za bunge. Hapa atasema si yeye bali bunge lanyewe limeamua, lakini ukweli utabaki nyuma ya pazia yupo huyu NAPE.
Hoja ya kuwa matangazo hayarushwi ili watu wafanye kazi haina mashiko, na haiingii akilini hata kidogo, kama ndivyo basi redio zote na vituo vyote vya TV vifungwe kuanzia saa mbili asubuhi na vifunguliwe saa kumi jioni ili watu wafanye kazi.
Sababu bunge ni kipindi kama kipindi kingine, na kila kipindi kina wapenzi wake na wafuatiliaje wake, na kila mtanzania ana kipindi chake, na vingi ya hivyo vipo ambavyo vinarushwa wakati wa kazi. Sasa wanataka kutuambia wafuatilaji wa bunge wasione bunge wakati wa kazi lakini wafuatiliji wa vipindi vingine kama vya Clouds 360 mathalan waendelee kukifuatilia hata kama charushwa wakati wa kazi? Leo uzinduzi wa daraja umerushwa live na mchana wa jua la utosi, hivi Nape alitaraji nani wa kutazama uzinduzi ule ikiwa watu wanatakiwa kuwa kazini?
Alafu kwanini wale ambao wako kazini au wanatakiwa wawe kazini wawakoseshe haki ya kufuatilia bunge watu wasio kazini? Msimamo wa Nape hauna mashiko, msimamo wake waturejesha maisha ya enzi ya kijima, maisha ya zama za kiza. Ni ajabu kwa waziri wa habari kusigina usambazaji wa habari. Nape ataka kuficha nini katika bunge????
Dotto Chamchua Rangimoto(Njano5)
whatspp/call 0622845394
Morogoro