Msikieni Shaffih Dauda kuhusu mauzo ya jezi za Yanga na Simba

canfi

JF-Expert Member
Jun 26, 2022
1,240
1,279
Tofauti na mitazamo watu

"Nikwambie ukweli kabisa kutoka moyoni mwangu jezi za Yanga kweli zinatembea, hasa jezi za njano na nyeusi. Jezi za Simba hazitembei kabisa kama jezi za kijani za Yanga, zinaenda taratibu sana."

"Yanga jezi zao ni bora kuanzia kwenye wazo, muundo na jinsi Yanga walivyo vizuri kwenye kufanya biashara. Hawatengenezi jezi kwaajili ya manufaa yao, wamejipanga mzingo ukipatikana unaenda kwa wakati, super dealer amejipanga vizuri msimu huu."
 
Yuko kwenye biashara ya jezi anajua zaidi lakini one thing kuhusu shaffih dauda, anamchukia sana Barbra na kuna watu kule ndani ya simba baada ya mirija kukatwa wako radhi hata kumpiga uchawi yule bibie awe chizi na shaffih dauda ni mtu wao hilo liko wazi.

Ndiyo maana anapoulizaga simba kuko shwari? anajua anachokisema kabisa, sema safari hii zengwe lake kama lile alilolifanya kwa Ramadhan Singano Messi naona linashindikana.

Tatu ,sitashangaa mauzo kuwa chini sababu mkanganyiko uliojitokeza na watanzania kuwa na mzuka team ikichukua ubingwa, upepo huo uko yanga kwa sasa ila mashabiki wa simba watakuwa hawamtendei haki vunja bei kafanya kazi nzuri sana mwaka huu jezi kali sana
 
Anasema haziuziki kwa kutumia data za kiduka chake? Jezi za simba zinauzwa kwa maduka ya vunjabei moja kwa moja na Sunderland K.koo kama muuzsji mkuu wa jumla.Lakini pia kuna mobile shops zinazunguka Nchi nzima,nani ahangaike kwenda kwenye kibanda chake kununua jezi wakati jezi zinapatikana kwa urahisi sana kila mahari kwa sasa.Akwende zake huko na mihasira yake ya kunyimwa tenda ya jezi.
 
Anasema haziuziki kwa kutumia data za kiduka chake? Jezi za simba zinauzwa kwa maduka ya vunjabei moja kwa moja na Sunderland K.koo kama muuzsji mkuu wa jumla...
Barbara katibua watu huko unambiwa kapitia mikataba yote ya usajili na mishahara kakuta MADUDU makubwa kuna watu wana share hadi mishahara na wachezaji, ni uchafu mkubwa sana, sasa wale wa teni pasenti kuna washkaji zake na huyu mhaya dauda, vita ni kubwa sana, huyu hatapumzika hadi ahakikishe kazua vurugu simba
 
Huyo mbwiga tumeshampuuza na genge lake
JamiiForums1029911400.jpg
 
Barbara katibua watu huko unambiwa kapitia mikataba yote ya usajili na mishahara kakuta MADUDU makubwa kuna watu wana share hadi mishahara na wachezaji, ni uchafu mkubwa sana, sasa wale wa teni pasenti kuna washkaji zake na huyu mhaya dauda, vita ni kubwa sana, huyu hatapumzika hadi ahakikishe kazua vurugu simba
Hilo la kuishi kwa 10% za mishahara ni mzoefu nalo sana.Hata pale Clouds vijana aliowaingiza pale wanampatia sehemu ya mishahara yao kila mwezi.Huyu huyu Shaffih alizuia mtoto mwenye kipaji kwenda nnje kucheza mpira matokeo yake akampachika yule toto bonge wake ambae hata kukimbia ni shida.Apeleke huko hasira zake Barbra keshaziba mianya yote,yeye aendelee kupiga mayowe huku mitandaoni.
 
ulisikia ile story ya ndondo cup mwaka jana fainali, team ya kina ali kiba na ile ya temeke kama sikosei.... sikuamini kama ile millions 20 mtu anataka apewe 10 la sivyo refa atawaminya , kina tegete walikuwa wakishika mpira ni filimbi tu wakafungwa sababu walikataa hilo sharti..nilivyoambiwa sikuamini lakini mmmmh
 
Rage hakukosea kabisa, na Mimi naongezea hapa...Tatizo lenu wengi ni Mbumbumbu, Shafii kauongea kitu kingine Mbumbumbu wako busy kumshambulia eti kakosa ulaji Simba, Yaani hata kwa kutumia akili za kuvukia barabara hata ya vumbi tu hili la jezi linahitaji mjadala? Na kwasasa Shafii na wengine wasifie kitu gani wakat Simba ipo kwenye mpito wa kukiweka kikosi chake vizur kama kile cha miaka 4 iliyopita.
Kuna muda jitahidini kauli ya Rage ifutike kwa vitendo.
 
Shafii alitamani kwa muda sana apewe nafasi Simba lakini Simba wakamkataa,kwaio sishangai kusikia akiponda mambo ya Simba.
Hivi hii tabia ya watu wa media ndyo wanapewa nafasi katika timu inatokea wapi, ina maana mtaani hakuna watu wenye skills za kupewa job kwa club hizi?
 
ulisikia ile story ya ndondo cup mwaka jana fainali, team ya kina ali kiba na ile ya temeke kama sikosei.... sikuamini kama ile millions 20 mtu anataka apewe 10 la sivyo refa atawaminya , kina tegete walikuwa wakishika mpira ni filimbi tu wakafungwa sababu walikataa hilo sharti..nilivyoambiwa sikuamini lakini mmmmh
Ni zake hizo hata sishangai kabisk.Katika project yoyote ukiona katia bichwa lake ujue tayari hapo keshawapiga pesa.
 
Dili la kuuza jezi za simba linamuma sana huyu kubwa jinga
Bichwa kubwa akili hana
Barbra kaza hapo hapo usiachie
 
Back
Top Bottom