Msigwa: Mabalozi wa nje hawana sifa ila wanachaguliwa kama zawadi na pole kwa makada wa CCM

Msigwa amesema mabalozi wanaochaguliwa hawana sifa bali wanachaguliwa kama zawadi au pole kwa makada watiifu kwa CCM.

 
Akisoma bajeti ya upinzani kwa wizara ya mambo ya ndani mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa amependekeza mabalozi wanaochaguliwa ni vyema wakachujwa kwa vigezo vya utendaji na sio kupewa kama zawadi au pole kwa makada wa CCM walioshindwa uchaguzi au kustaafu kama inavyofanyika sasa hivi

PENGINE INGEPENDEZA ZAIDI KAMA MCHUNGAJI ANGETUELEZA BAYANA SIFA ZA KUWA BALOZI NI ZIPI ULIMWENGUNI KOTE NA HAPA KWETU NI ZIPI ILI TUWEZE KUJUA. hizi hadithi zisizokuwa na mshiko zitolewazo mahala kama bungeni ni ishara kuwa kuna wakati hawa wateule wetu huwa hawana la maana la kuongea ila watapenda waonekane kuwa wao ni magwiji kwa kuongea bungeni.
 
Hakuna Serikali duniani inayowapa wapinzani nafasi Za kitendaji kama hizo. Mwisho wao ni uwaziri duniani kote.

Anamanisha na Duni Au Lowassa apewe kwa vile walishindwa?
 
Ni kweli kabisa asilimia kubwa ni wale walioshindwa majimboni, Je swali la kujiuliza kile chuo cha diplomasia pale kurasini kila mwaka kinatoa wahitimu, Je wahitimu waoasoma pale na kufaulu vizuri wanafanya nn hakuwa wahitimu wanaoweza kuwa mabalozi nje ya nchi wachilia mbali kuwa maafisa wa ubalozi.

Tuchukulie mtu kafanya kazi serikalini amestafu badala ya kuacha apumzike anapewa ubalozi nje ya nchi hawa vijana waliosoma chuo cha diplomasia wanakwenda wapi??? wanafanya nn wasipelekwe kuwa mabalozi?

Umefanya kazi umestaafu pumzika wachie wengine nao wafanye kazi jamani!! Kila kukicha tunalalamika ajira hakuna wakati ajira zipo ila zinapewa wengine kama bonus na pole ya kutoswa jimboni kweli haipendezi huu utaratibu ubadilike jamani hata sie hohehahe tuliosoma ka pesa ya kobonda kokoto,kulima vibarua tuweze kupata ajira sio wale wa full AC lami mpaka sebuleni wao ndio wakupewa hizo ajira, TANZANIA NI YETU SOTE tuondoe hili tabaka la walio nao na wasionao, mtoto wa msukuma mkokoteni kariakoo nae akawe balozi nje ya nchi aone raha ya kupinda mgongo na kusoma kwa shida ikoje
 
Hakuna Serikali duniani inayowapa wapinzani nafasi Za kitendaji kama hizo. Mwisho wao ni uwaziri duniani kote.

Anamanisha na Duni Au Lowassa apewe kwa vile walishindwa?
nope, anamaanisha wawe wanatoa kwa watu kutokana na uelewa wao wa mambo na sio kulipa favour
 
Wote walioteuliwa hawana sifa?
Nani hana sifa ya kuwa balozi ambao rais kawateua?
Hilo ndio hoja ya msingi
 
Kasema ukweli kabisa yan mabalozi wote wanateuliwa kama tunzo na chama chao wenyew husema utapangiwa kazi nyingine
 
Halafu serikali ikianza kuwachuja mabalozi utamskia Msigwa akilalamika. Vigumu kuamini wanachosema hao wabadili gia angani.
 
Halafu serikali ikianza kuwachuja mabalozi utamskia Msigwa akilalamika. Vigumu kuamini wanachosema hao wabadili gia angani.
Huwa hamtaki kuambiwa ukweli na mnang'ang'ania TU kale ka wimbo cha JEHANAMU au KUZIMU oooooh ni ile....ile......mtaisoma namba......
Nilishwahi kusema hakuna JIPYA tutategemea kutoka awamu hii au series hii ya CCM, maana wao wenyewe walisha KIRI kuwa ni ile ile.......now what NEWS do we expect???????????
 
Back
Top Bottom