Msiba wa George Kahama wamkumbusha Mhariri wa Raia Mwema, Abdulwahid Sykes

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,791
31,804
uho85zSY51TvwDNhukm1-qw8Ps5P-cH5vBfx_ATJWLWrgobedeL4YiMZAiCX8L7nv50KLdt9rosSoioMBMltqJYikid8b7XhmkVKx0mU2ptd5piTZivpuuSRObVQLVWAMWS3WrfrVrMc2XtRur8OuuuT97YvDCz_FLbmAfADpmxz59XfhPBkEHvoA6Pe8NW9UGXxyzPVVUsVR_B6Imj1uPwacYrBvuxyxk6YnFQLYXTiQ387YskRmlPP0aXHpbaTvnwsj3sIN2na5oDGNCm433TFEJFWZXu-dQ5234WjqER_5nthekIXNRQVEk6qbFchotMcEVXQEntwaeg2UByEtQ8ESg-MzDFzVOf2JGX_JCsgD3iM2OSAoG9-YPxk9CqjDFcvSHyIY79F0KMEanispoSpMVplT6jsk0oYvODo78bG7WbwKnxX_WRX-gE0U6-jxcHTumcRbNiILVzuaHhedx8_8MzX243L4o4_yewpvqMnlTOvpElOPGEi6q1tXQo5eW-Vum1RgBVtjfLuQs0s_h2xESUpSz5gLAPZJxPJo823xnDQ_UivReb3867uVTKsPY6mS3euGFNt9N4eMy5_qovrv8gXJhkwcRPWCeeJMOcfCXb8Nw=w299-h692-no

Mhariri wa Raia Mwema katika toleo lake la 15 - 21, Machi 2007 katika tahariri yake kwa kumuadhimisha marehemu George Kahama aliyezikwa jana ameeleza masikitiko yake kwa Tanzania kutokuwa na historia ya mashujaa wake. Mhariri kamtaja pamoja na wazalendo wengine Abdul Sykes kama mmoja wa wazalendo ambae historia ya mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika bado haujathaminiwa.

Binafsi nimefarajika kuwa kumbe si mimi peke yangu ninayoona upungufu huu katika taifa letu.

Mara ya kwanza mwaka wa 1988 gazeti la Africa Events lililokuwa likichapwa London lilipochapa makala yangu, ''In Praise of Ancestors,'' na nikamtaja marehemu Abdul Sykes kwa sifa ya kuaisi chama cha TANU 1954, toleo zima lilikusanywa na kutolewa katika mzunguko.

Mambo hayakuishia hapo toleo la gazeti hilo lililofuatia ilichapwa barua kutoka CCM Makao Makuu Dodoma iliyoandikwa na kada mashuhuri wa wakati huo na aliyekuwa na cheo kikubwa katika Sekretariati ya Kuhamasisha Umma iliyokuwa na vitisho na dharau dhidi yangu. Kisa na kosa langu kumtaja Abdul Sykes na wazalendo wengine na kusema kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika haiwezi kutenganishwa na mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Alipokufa Dossa Aziz katika maziko yake Mlandizi hakuna katika viongozi wa CCM aliyekuwapo pale mazikoni aliyejua Dossa alikuwa nani kwa Mwalimu Nyerere wala kwa TANU yenyewe na kwa bahati mbaya sana Nyerere hakuhudhuria maziko yale. Labda angekuwapo angemueleza Dossa alikuwa nani kwake na kwa TANU.

Alipokufa Paul Bomani mambo hayakuwa tofauti na yale ya maziko ya Dossa Aziz. Hakuna katika viongozi wa CCM aliyejua mchango wa Bomani.

Hawa wazalendo watatu niliowataja hapa kwa uchache wote wanaunganishwa na sifa moja adimu sana. Hawa walitajirika katika ukoloni na TANU ilipoasisiwa walikuwakuwa tayari wana na fedha zao. Hawa hawakutajirikia katika TANU. Wazalendo hawa walitoa fedha nyingi kwa TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kwa kuhitimisha ningependa kusema kuwa hakika nimefarajika sana kuwa kumbe kuna wenzagu na wao wameona upungufu wa jambo hili.

Kwa kuitika mwito wa Mhariri wa Raia Mwema itapendeza kama katika jengo jipya la CCM pale Patrice Lumumba Avenue CCM ikaanza kutafuta historia ya mashujaa wetu na kuwaenzi angalau kwa kuweka picha zao na maelezo mafupi.

Kizazi hiki cha leo kingependa kuona picha ya Sheikh Suleiman Takadir na maelezo yake ya mchango wake katika kudai uhuru wa nchi yetu, picha ya Saadan Abdul Kandoro, Hamza Mwapachu, Bi. Titi Mohamed na Tatu biti Mzee, Iddi Faiz Mafungo, Mshume Kiyate kwa kuwataja wachache na huko mikoani na wilayani haya yafanyike.

Hapo Makao Makuu ya CCM Dodoma ziwekwe picha za Omar Suleiman, Haruna Taratibu, Edward Mwangosi, Tanga zikwekwe picha za Abdallah Rashid Sembe, Bi. Mwanamwema, Hamisi Heri. Lindi picha za Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Sheikh Yusuf Badi. Kilimanjaro waweke picha za Eikaeli Mbowe, Yusuf Olotu, Juma Ngoma, Mama Biti Maalim, Halima Selengia.

Bukoba waweke picha za Ali Migeyo, Suedi Kagasheiki, Abdallah Rutabanzibwa nk. nk.

Tusitishike na majina haya ya Kiislam kwani hii ndiyo historia yenyewe hatutoweza kuibadili.
 
kuna kitu sikukifuraga Sir George Kahama alikwa mbunge wangu kule karagwe kipindi cha mkapa,sasa kisa cha kuzikwa kinondoni,najua wilaya ya karagwe imetoa watu maarufu wengi sana ila huyu alikuwa ndo icon yetu,kumzika dsm ni kufuta historia yake wilayani alipozaliwa
 
Wazee wako wa Gerezani walifanya kosa kubwa sana la kumuachia Kambarage chama na hayo unayoyalalamikia hapa ndiyo matokeo yake.
Kitulo,
Mimi silalamiki ila naeleza historia kama ilivyokuwa.

Wala wazee wetu hawakufanya kosa lolote katika
kumwingiza Mwalimu Nyerere katika TANU.

Huu umoja unaozungumzwa na wanasiasa wetu
ulianza hapo.
 
Mzee wangu Mohamed Said basi jitahidi kuwa una balance mabandiko yako, Usindeshwe na UDINI. Nimeshangazwa kuwa Bukoba waweke picha za Ali Migeyo, Suedi Kagasheiki, Abdallah Rutabanzibwa nk. nk. Wakazi wa Bukoba hatuwatambui hao kabisa kihistoria wakati wa kupigania Uhuru. Labda walipigania Uislam.

Napenda sana kukusoma, lakini punguza udini.
 
Chachu...
Siwezi kushangaa ikiwa hamumtambui Ali Migeyo.

Hakutambuliwa Abdul Sykes mwenye kadi ya TANU No. 3
Hakutambuliwa Ally Sykes mwenye kadi ya TANU No. 2 na
kadi ya TANU No. 1 ya Mwalimu Nyerere ni Ally Sykes
ndiye aliyeiandika.

Hajatambuliwa baba yao Mzee Kleist aliyejenga hiyo ofisi
ilipozaliwa TANU 1954.

Hajatambuliwa Iddi Faizi Mafungo aliyesimamia safari ya
Nyerere UNO 1955.

Kipi mimi leo kitanishangaza ikiwa hamumtambui Suedi
Kagasheki?

Ama kuhusu Uislam naam ulitumika sana katika kupambana
na ukoloni kuanzia Vita ya Maji Maji dhidi ya Wajerumani hadi
kudai uhuru kutoka kwa Waingereza.

Ilikuwa Salum Mpunga na Ali Ibrahim Mnjale ndiyo vijana
waliomleta Mwalimu Nyerere Jimbo wa Kusini kuja kupambana
na Kanisa lililokuwa linawatisha wananchi kujiunga na TANU kudai
uhuru.

Wala katika kuandika historia hii hakuna udini ni historia tu tupu
iliyokuwapo hatuwezi kuifuta hata kama kuna baadhi yetu kwa
sababu zetu binafsi hatuipendi.

Kipi kitanishangaza ikiwa wewe leo hii humjui Sheikh Yusuf Badi,
Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir
waliokuwa
mstari wa mbele kupigania uhuru wa Tanganyika?

Ikiwa wewe una historia nyingine isiyokuwa hii tuwekee hapa Majlis
tuisome.
 
Mzee wangu Mohamed Said basi jitahidi kuwa una balance mabandiko yako, Usindeshwe na UDINI. Nimeshangazwa kuwa Bukoba waweke picha za Ali Migeyo, Suedi Kagasheiki, Abdallah Rutabanzibwa nk. nk. Wakazi wa Bukoba hatuwatambui hao kabisa kihistoria wakati wa kupigania Uhuru. Labda walipigania Uislam.

Napenda sana kukusoma, lakini punguza udini.
Chachu hebu sikiza hii video nimemzungumza Ali Migeyo huenda
ikakusaidia kujua historia ya TANU:
 
Msiba wa George habari za Sykes ???:eek::cool:
Mlaleo,
Ingekuwa si msiba wa George Kahama Mhariri wa Raia Mwema
asingeandika tahariri ile na kumtaja Abdul Sykes.

Wewe ni mgeni katika historia hii lakini nitakueleza historia hii.

Jina la Abdul Sykes lilifutwa katika historia ya TANU na historia
ya kudai uhuru wa Tanganyika.

Jopo la waandishi wa historia ya TANU iliyoandikwa na Chuo Cha
Kivukoni lilikataa kupokea ''notes,'' za Hassan Upeka kuhusu
Abdul Sykes ambazo zingesaidia uandishi wa historia ya TANU.

Hii maana yake ni kuwa Abdul Sykes hakutajwa katika kitabu
kile.

Kwetu sisi hakuna awezae kuandika historia ya TANU na historia
ya uhuru wa Tanganyika bila kutaja jina la Abdul Sykes.

Wala hakuna mtafiti awezae kuandika historia ya Mwalimu Nyerere
bila ya kutaja jina la Abdul Sykes na nduguye Ally.

Brendon Grimshaw aiyekuwa mhariri wa Tanganyika Standard
mwaka 1968 alipoandika taazia ya Abdul Sykes baada ya kifo chake,
taazia ile haikuwafurahisha baadhi ya watu pale Makao Makuu ya
TANU.

Haikuwafurahisha viongozi hawa wa TANU mpya kwa kuwa alisema
pamoja na mambo mengine kuwa Abdul Sykes ndiye mwasisi wa
TANU.

1986 Paula Park mwanamke wa Kiingereza akiliandikia gazeti la Africa
Events aliombwa kuondoka nchini baada ya mahojiano na Ally Sykes
na akaandika yake aliyoandika Grimshaw [/B]1968.

1988 gazeti hilo hilo la Africa Events liliondolewa katika mzunguko kwa
kuchapa makala niliyoandika na ndani yake nikamtaja Abdul Sykes na
mchango wake katika kuasisi TANU.

Sasa narudi kwako hilo swali ulilouliza.
Makala ya Kahama anatajwa Sykes.

Naam.

Sikutegemea kama itakuja siku gazeti la hapa nyumbani litamtaja Abdul
kama mzalendo aliyepigania uhuru wa Tanganyika na anastahili kuenziwa.

Ikiwa una swali jingine usisite kuniuliza.
 
Ndugu Mohamed Said, wote uliowataja(waislam) walishiriki vizur kuusaka uhuru wa Tanganyika. Hata mimi niliwahi kusoma kwamba ktk vikao vya hao waasisi jina la TANU lilitungwa na Sykes. Kasoro ni pale unapoonyesha kana kwamba uislam wao ndio uliochangia.Ni kama ungependa taifa lipigie mstari ushiriki wa waislam ktk kuleta uhuru. Mimi nilikuwa msomaji wa African Events. Lilikuwa na mtazamo huohuo. Huo si mtazamo mzuri wala sahihi Hata akina Kinjeketile na Bushiri hawakupigana vita kwa sababu ya uislam. Wao walipinga kutawaliwa. Hebu tusilee udini ktk nchi yetu. Tushukuru Mungu chembe za udini zinazoibuka sasa zilizimwa mapema na akina Nyerere.
 
  • Thanks
Reactions: Pep

Joseph...
Unajaribu kutaka kufanya mjadala na mimi katika somo ambalo
huna ujuzi.

Ikiwa utapenda naweza nikakupa rejea za kusoma ili ulijue tatizo
la udini na nani walikuwa wahusika wakuu.

Anza na Bergen (1981).
Sivalon (1992).
Njozi (2002).

Ikiwa utapenda msome Said (1998).
 
Mlaleo,
Ingekuwa si msiba wa George Kahama Mhariri wa Raia Mwema
asingeandika tahariri ile na kumtaja Abdul Sykes.

Wewe ni mgeni katika historia hii lakini nitakueleza historia hii.

Jina la Abdul Sykes lilifutwa katika historia ya TANU na historia
ya kudai uhuru wa Tanganyika.

Jopo la waandishi wa historia ya TANU iliyoandikwa na Chuo Cha
Kivukoni lilikataa kupokea ''notes,'' za Hassan Upeka kuhusu
Abdul Sykes ambazo zingesaidia uandishi wa historia ya TANU.

Hii maana yake ni kuwa Abdul Sykes hakutajwa katika kitabu
kile.

Kwetu sisi hakuna awezae kuandika historia ya TANU na historia
ya uhuru wa Tanganyika bila kutaja jina la Abdul Sykes.

Wala hakuna mtafiti awezae kuandika historia ya Mwalimu Nyerere
bila ya kutaja jina la Abdul Sykes na nduguye Ally.

Brendon Grimshaw aiyekuwa mhariri wa Tanganyika Standard
mwaka 1968 alipoandika taazia ya Abdul Sykes baada ya kifo chake,
taazia ile haikuwafurahisha baadhi ya watu pale Makao Makuu ya
TANU.

Haikuwafurahisha viongozi hawa wa TANU mpya kwa kuwa alisema
pamoja na mambo mengine kuwa Abdul Sykes ndiye mwasisi wa
TANU.

1986 Paula Park mwanamke wa Kiingereza akiliandikia gazeti la Africa
Events aliombwa kuondoka nchini baada ya mahojiano na Ally Sykes
na akaandika yake aliyoandika Grimshaw [/B]1968.

1988 gazeti hilo hilo la Africa Events liliondolewa katika mzunguko kwa
kuchapa makala niliyoandika na ndani yake nikamtaja Abdul Sykes na
mchango wake katika kuasisi TANU.

Sasa narudi kwako hilo swali ulilouliza.
Makala ya Kahama anatajwa Sykes.

Naam.

Sikutegemea kama itakuja siku gazeti la hapa nyumbani litamtaja Abdul
kama mzalendo aliyepigania uhuru wa Tanganyika na anastahili kuenziwa.

Ikiwa una swali jingine usisite kuniuliza.
Alifutwa kwa kuwa hakuwa na adabu hivyo upuuzi wake wa kuleta udini ndio sababu kuu.... hata wewe utafutika kwasababu ya udini udini wako kwanza unachosha tu
 
Ndugu Mohamed Said, wote uliowataja(waislam) walishiriki vizur kuusaka uhuru wa Tanganyika. Hata mimi niliwahi kusoma kwamba ktk vikao vya hao waasisi jina la TANU lilitungwa na Sykes. Kasoro ni pale unapoonyesha kana kwamba uislam wao ndio uliochangia.Ni kama ungependa taifa lipigie mstari ushiriki wa waislam ktk kuleta uhuru. Mimi nilikuwa msomaji wa African Events. Lilikuwa na mtazamo huohuo. Huo si mtazamo mzuri wala sahihi Hata akina Kinjeketile na Bushiri hawakupigana vita kwa sababu ya uislam. Wao walipinga kutawaliwa. Hebu tusilee udini ktk nchi yetu. Tushukuru Mungu chembe za udini zinazoibuka sasa zilizimwa mapema na akina Nyerere.
Nimemsikiliza vizuri sana Mzee Mohamed Said hajasema mahali popote kuwa ni waislam tu waliopigania uhuru ila amesema majority walikua ni waislamu na huo ukweli kabisa ila kwaa watu kwa makusudi wamewafuta kwenye historia kama huyu mzee Ally Sykes..mimi nilimpinga kidogo Mzee Mohamed Said hapo mwanzo lakini baada ya kusikiliza hii video yake nimegundua anayosema ukweli mtupu ila kuna watu wamepindisha historia sijui kwa manufaa ya nani. Na ni ukweli usiopingika ni waislam ndio walikua mstari wa mbele kuipigania uhuru wa Tanganyika na wala huu sio udini ila FACTS.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom