Msiba na namna ya kumsindikiza marehemu, utamaduni uliozoeleka

Mto_Ngono

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
686
589
'waache wafu wawazike wafu wenzao' maneno haya ya kwenye maandiko yanamaanisha hatutakiwi kuhangaika sana na wafu au marehemu kwa sababu wameshamaliza muda wao na hakuna kitu kinachoweza kuongeza thamani yake au kupunguza aliyokuwa nayo wala kufanya chochote juu yake kitakacho punguza makosa yake au kuongeza. Akishafariki ni kuzika mara moja.

Zipo tamaduni mbalimbali za kumsindikiza marehemu katika nyumba yake ya milele.

Waislam huzika siku hiyo hiyo wenda itokee sababu iliyo nje ya uwezo na kusababisha kuzika kesho yake.

Wakristo hukaa na msiba hadi siku 5 inategemeana tu na sababu nyingi kama uwepo wa ndugu n.k lakini kiufupi hukaa na msiba siku nyingi sana.

Nimeainisha utaratibu huo katika makundi hayo lakini sidhani kama kuna haja ya kukaa na marehemu kwa muda mrefu sana najua inauma sana lakini ameshakufa ni vizuri kumpumzisha mapema.

Napenda sana utaratibu wa kiislamu wa namna ya kudeal na msiba. Hawakai nao na huzika haraka lakini kwa namna ya kikristo hukaa na msiba muda mrefu ambapo si vizuri kwanza unaongeza gharama na kuingia gharama kubwa kulisha au kwa namna yoyote kuugharamia hadi muda wa maziko ufike, pili unaongoza uchungu na huzuni kwa waombolezaji na hii yatokana na mawazo yaliyopo juu ya uwepo wa mwili kabla ya kuzika na mwisho, muda wa kushughulika na msiba waweza kupoteza opportunity zingine za kuwaongezea kipato au kupoteza mapato kutokana na kufunga biashara muda mwingine.

Katika makundi hayo juu, wapo wengine ambao huonesha utamaduni mzuri ambao hawaweki matanga kwa siku nyingi pia hata namna ya kuzika hawakusanyiki wengi wanakuwa wachachekwa ujumla suala la kumpumzisha marehemu huwa rahisi na la muda mfupi na wamalizapo huendelea na shughuli kama kawaida. Mifano ipo mingi lakini twaweza kuangalia desturi kwa white men (western culture). Tunaweza kuwaita wabinafsi na wachoyo kwa kulinganisha namna zetu za kushughulika na misiba lakini naamini yaweza kuwa njia nzuri na rahisi isiyokuwa na gharama kubwa wala ugumu kuikamilisha.

Nadhani kuna haja ya kubadilisha utamaduni huu ili kuenzi maneno ya wafu kuwazika wafu wenzie. Kufanya sehemu ya msiba sio ya watu kushinda bali kutoa pole na kwenda kuzika then kila mtu kugawanyika. Kwa kufanya hivyo twaweza okoa mambo mengi.

Waweza kuwa na maoni tofauti ila yangu ni haya. Ni jambo la huzuni na linauma lakini sio lazima likafanyika kutokana na mazoea. Sorry kwa nitakao wakwaza.
 
Mkuu usijifananishe na wazungu wao walisha abolish mambo ya ukoo etc tangu karne ya 4 ndo mana kimsingi wazungu ni wabinafsi ni yeye na familia yake au watu wake wa karibu mzungu waweza ishi nae flat moja floor moja miaka hata 7 na msijuane kabisa, tuishi kama tulivyo kwa wakisto mtu akifa leo ukisema umzike kesho watakushangaa watu wetasema walimchoka marehemu etc waislamu wao dini yao ipo hivyo na hua hawana complications...
 
Lakini nadhani japo ni wabinafsi wana utaratibu mzuri na ndo maana wanaendelea kwa haraka. ila hata tukifuata namna waislam wafanyavyo ni vizuri zaidi. uwekaji wa msiba kwa siku hizo zote nadhani sio vizuri kwa sababu nilizotoa hapo juu.
 
Haya in mawazo yk were ndugu .huwezi lazimisha watu et duniani wawaze wazo moja hiyo haiwezekani.mbona hupingi uumbaji was mungu wako warefu wafupi wanene weupe nk.mbona hujawaza dunia ilivyo kuna sehemu kn baridi au joto kuna sehemu kuna jangwa nk.usilazimishe mila za wamasai ziwe km wasukuma.tofauti zote hz mungu ameziweka Ili utukufu was mungu update kujidhihiri kwa wanadamu.ukitaka kutafiti kila kitu duniani hutaweza.suala LA waislamu kuzika Siku hiyo by lilitokana na mazingira ya kijografia so LA kiimani.
 
Yote ni mawazo tu na ushauri ambao sio kila mtu auchukue. Huu ni muendelezo wa tathmini ya kwa nini 'mambo haya yafanyike hivi na yale vingine' zipo thread ambazo nishaandika Mungu na Uumbaji..Sababu nilizotoa za kwa nini kumsindikiza marehemu kusichukue siku nyingi zinasindikiza kile nachoamini.
 
uislamu ndo mfumo sahihi wa maisha
umeweka wazi kila kitu
Muhamad ( s.a.w) ni mjumbe wa kweli wa Mungu
Jadili mada naona unatoka nje ya mada mkuu hatuzungumzii dini ipi ni nzuri na ipi c nzuri kinachojadiliwa hapa ni 'utamaduni' wa kushughulikia wafu.
 
Jambo la kuzika haraka haraka kwa ndugu zetu waislam chimbuko lake ni Uarabuni ambako kama mjuavyo hali ya joto kali jangwani inasababisha mwili kuharibika haraka,kwa hiyo dawa ni kuzika chap chap.
 
Waislam wameamrishwa mambo matatu yafanyike kwa haraka sana.
1. Kuzika.
2. Kufunga ndoa
3. Kusilimisha
Huo ni utamaduni wa mashariki ya kati hata kabla ya uislamu kuja.

Hata Yesu Kristo alizikwa siku hiyo hiyo aliyokufa akafufuka siku ya tatu kama ilivyoandikwa.
 
Mimi binafsi napenda utamaduni wa kuzika baada ya siku 2 sababu kwanza anaezikwa ni binadamu sio kama mnyama unamjimbiza shimoni upesi asinuke.

Kipindi hicho kinawapa fursa ya kumtafakari mpendwa wenu kwa kina na kinatoa hali fulani kwamba kuna kitu cha tofauti kimetokea kisicho cha kawaida.

Kuhusu hali ya uchumi hilo ni la mtu binafsi sio wote wanashindwa kugharamia misiba yao.
 
Vipi ule utamaduni wa kuwazuia wanawake wasiende makaburini(kuzika).
Nao pia ufuatwe au haufai??
 
Lakini nadhani japo ni wabinafsi wana utaratibu mzuri na ndo maana wanaendelea kwa haraka. ila hata tukifuata namna waislam wafanyavyo ni vizuri zaidi. uwekaji wa msiba kwa siku hizo zote nadhani sio vizuri kwa sababu nilizotoa hapo juu.
Hao waislam pamoja nankufanya hivyo wameendelea sana au
 
Lakini nadhani japo ni wabinafsi wana utaratibu mzuri na ndo maana wanaendelea kwa haraka. ila hata tukifuata namna waislam wafanyavyo ni vizuri zaidi. uwekaji wa msiba kwa siku hizo zote nadhani sio vizuri kwa sababu nilizotoa hapo juu.
Hata Waislamu hufanya msiba kwa siku kadhaa isipokuwa mzishi ndio hufanywa haraka.
 
Hakika utaratibu wa kukaa na maiti muda mrefu si mzuri sababu kwanza lazima tuelewe mtu akifa ameishakufa hata tukae nae mwaka atabaki kuwa amekufa tutazidi kujiongezea maumivu tu, pili siku hizi msiba ni gharama kwa mfiwa watu wanaamka asubuhi wanapiga tea wanasepa, wanarudi mchana au jioni tena wanarekebisha hizi gharama asilimia kubwa zinatoka kwa mfiwa.Sasa nimetambua busara ya Wazee wa zamani mfano kijijini kwetu ilikuwa unapotokea msiba chakula ni kande na mahindi hayakobolewi ili watu watofautishe msiba na sherehe
 
Back
Top Bottom