Mshauri wa Donald Trump kuhusu usalama Michael Flynn ajiuzulu

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
Mshauri mkuu wa ikulu ya White House kuhusu usalama wa taifa Michael Flynn amejiuzulu kuhusiana na uhusiano wake na maafisa wa Urusi, vyombo vya habari Marekani vinaripoti.

Bw Flynn anadaiwa kujadili vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi akiwa na balozi wa Urusi kabla ya Rais Donald Trump kuingia madarakani.

Anadaiwa kuwapotosha maafisa wa utawala huo mpya kuhusu mazungumzo yake na balozi huyo.

Awali, vyombo vya habari Marekani viliripoti kwamba Wizara ya Haki ilitahadharisha ikulu ya White House mapema kuhusu mawasiliano ya Flynn na maafisa wa Urusi mwishoni mwa mwezi uliopita.

Walisema Bw Flynn huenda akashurutishwa kuwa kibaraka wa urusi.

Maafisa wakuu wa chama cha Democratic walikuwa wametoa wito kwa Bw Flynn kuachishwa kazi.

Mashirika ya habari ya Associated Press na Washington Post yanasema wizara ya haki Marekani ilitahadharisha kuhusu kile ilichosema ni mambo aliyoyasema Bw Flynn kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Urusi.

Ni kinyume cha sheria kwa raia wa kawaida kujihusisha na shughuli za kidiplomasia Marekani.

Mazungumzo kati ya Flynn na balozi wa Urusi yanadaiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka jana, kabla ya Bw Flynn kuteuliwa kuhudumu katika uatawala wa Bw Trump.

Bw Flynn, ni luteni jenerali mstaafu.

Awali alikana kuzungumza kuhusu vikwazo dhidi ya Urusi na balozi huyo, na Makamu wa Rais Mike Pence pia alijitokeza hadharani kumtetea.

_94636045_hi037879843.jpg

Bw Flynn baadaye aliambia maafisa wa White House kwamba kuna uwezekano yeye na balozi huyo walizungumzia vikwazo hivyo.

Gazeti la Washington Post lilisema Kaimu Mwanasheria Mkuu Sally Yates aliambia White House kwamba mshauri wao mkuu wa usalama wa taifa "alijiweka katika hali ya hatari" kwa kuzungumza na Warusi kabla yake kuruhusiwa kisheria kufanya hivyo na kwamba Wizara ya Haki ilifahamu kwamba alimpotosha Bw Pence.

Mwezi uliopita, Bi Yates alifutwa kazi na Bw Trump kwa kukataa kutetea marufuku yake dhidi ya raia wa mataifa saba yenye Waislamu wengi kuruhusiwa kuingia Marekani.
 
That guy was a mole, they got him. He was fired by the Obama administration, remember?

Ila issue ilikuwa personal kwake
Affair
Ila ngoja tuone atawekwa nani
Huyu Fylnn kakwepa kuambiwa you are fired
 
A pair of Democratic lawmakers -- Reps. John Conyers, Jr., top Democrat on the House Judiciary Committee, and Elijah Cummings, top Democrat on the House oversight Committee -- sent a request for a "full classified briefing" on the circumstances surrounding Flynn to the Justice Department and FBI Monday night following Flynn's resignation.
"We in Congress need to know who authorized his actions, permitted them and continued to let him have access to our most sensitive national security information despite knowing these risks. We need to know who else within the White House is a current and ongoing risk to our national security," they wrote in a statement.
 
Vulnerable to BLACKMAIL with the Russians, halafu si wa mchezo mchezo.
He's a TOP NATIONAL SECURITY ADVISER.

Asee!
 
Ndio watu wajue kuwa ukiwa kiongozi sio kila unayekutana naye mnaongea tuu,kiongozi unafuatiliwa,unachunguzwa na unalindwa hivyo kujiheshimu ni muhimu sana na kupenda kusema ukweli siku zote ni muhimu sna.
 
Huu mwanzo huu ni shida. Pence nae akaingia kingi halafu akamtetea.
Hata kama ilitokea before they took over the WH, Dems wataanza ku question zaidi relationship kati ya Trump, sec of state wakeTillerson na ukaribu wake kwa Putin.

Pence alimtetea si Mara moja basi, kumbe jamaa wanamwangalia tu! Trump alikuwa anajua mchezo wote aliokuwa anaucheza Michael Flynn, Pence alikuwa gizani! Wakamchomekea nae akaenda kubwabwaja kwenye Meet The Press! Hii kitu itaibua mambo mengi sana, hasa business ties and dirty money kati ya Trump na Russians! Hebu jiulize ni kwa nini mpaka leo hataki kutoa forms zake za mambo ya tax returns kwa public?
 
Pence alimtetea si Mara moja basi, kumbe jamaa wanamwangalia tu! Trump alikuwa anajua mchezo wote aliokuwa anaucheza Michael Flynn, Pence alikuwa gizani! Wakamchomekea nae akaenda kubwabwaja kwenye Meet The Press! Hii kitu itaibua mambo mengi sana, hasa business ties and dirty money kati ya Trump na Russians! Hebu jiulize ni kwa nini mpaka leo hataki kutoa forms zake za mambo ya tax returns kwa public?


Hapo sasa. Kitu kingine cha kushangaa ni kuwa, he's a former general so he knows better especially kwenye issue sensitive kama hii, mtu hawezi kuongea tu anavyopenda. Sijui alipata wapi ujasiri wa kuingia mzima mzima, unless kuna mengi nyuma ya pazia.
 
Back
Top Bottom