Mshahara ni kiasi gani

Lio 002

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2014
Posts
436
Reaction score
68
Habar wana jf mm ni muhitimu wa ngazi ya Diploma in Marketing management nimeitwa kwenye interview kampuni moja hivi siku ya juma tatu sasa nilikuwa naomba munifahamishe kiwango sahihi cha mshahara kwa mtu aliye na diploma ya marketing management ntashukuru sana wana jf kwa mawazo yenu
 
Swala la mshahala lilinifanya nikose kazi wakati Fulani nilipo ulizwa ni kiasi gani ningependa kulipwa nikaropoka et kwasababu nilijiona Nina taaluma hyo Nina uzoefu wameniita nikaona niropoke ili nifaidi kumbe looooo nilijiponza... nakushauri wakikuuliza kuhusu mshahara usiseme wewe waulize kiwango chao then unaweza kutoa ombi narudia tena OMBI ili uongezewe wanaweza kukufikiria usithubutu kufanya mbwembwe za mshahara utakosa Kazi... ASANTE..
 
Kwa kukushauri,mimi nipo kwenye hii industry,mara nyingi kinachoangaliwa ni uzoefu na nini ulikionyesha kwenye interview yako,wakati wa probation ndio hasa huwa tunapanga kiwango halisi kutokana na muenendo wako kipindi hicho.Diploma au degree kwenye level ya kawaida ambayo siyo managerial level mishahara ya kuanzia mara nyingi ipo sawa,kwa sababu tunaamini matokeo ya kwenye makaratasi siyo ya kwenye field. Pia kampuni zinatofautiana,kuna ambazo unapewa target na ukifikia unapata commission lakini basic inakuwa ndogo,na kuna nyingine mshahara ni hicho peke yake.Pia tunaangalia other benefits,like mawasiliano usafiri na hata nyumba,kuna kampuni zinatoa zingine hazitoi. Zaidi, private sector hasa upande wa sales & marketing haina ngazi ya mshahara kuendana na elimu (ingawa elimu ni muhimu zaidi). Sasa nitakupa mfano wa kampuni yetu ambayo ni ya kizawa na inajihusisha na bidhaa zitokanazo na petroli,Dip-Degree starting basic Tsh 450,000 pembeni kuna mawasiliano na gharama za usafiri,elimu hiyo hiyo uzoefu zaidi ya 2 years (ukiwa kwetu) Tsh 690,000 hapo ni tofauti na managerial level. Nimetoa hiyo kukusaidia upate angalau picha kidogo (kuwa usitegemee kuwa wataangalia elimu bali uzoefu na jinsi unayoelewa marketing in general)
 
Mhhhhh mbna kazi ninayo aiseee hyo j3
 
maelezo mazuri umepewa hapo juu fuatilia, kwahiyo we hapo wambie tu upo tayari kupata mshahara wowote, kwa kuwa unataka kuendeleza career yako. mimi nimefanya usahili mara 2, private sector ambayo nilipata kazi, hilo swali niliulizwa zaidi ya mara 4 tena wanakomalia kweli ujibu, ila mimi nilikomaa sijawajibu wala nini, wakasema basi, wakaniita kazini nikaukuta safi tu, mawasiliano kila mwezi, usafiri, field nyingi, dili, yani ukijumlisha maisha yanaenda, maana hata ukitaja mil 2 mshahara hautoshi. ya 2 serikalini hilo swali hamna maana unajulikana.
 

Kwa hyo niwaambye wanipe mshahara wowote au sio?
 
Kwa mm nadhani kutokana na gharama tofauti za maisha mnaonaje kama nikisema ni laki sita kwa mwezi?
 
Kwa mm nadhani kutokana na gharama tofauti za maisha mnaonaje kama nikisema ni laki sita kwa mwezi?

na kama jiyo kampuni gross ikawa 450,000 au 500,000 huoni kuwa tayari umekosa kazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…