Mshahara Mwalimu wa Seminary

MENISON

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2013
Posts
726
Reaction score
623
Wadau naomba kujua mshahara wa mwalimu wa a level physics shule za seminary, wiki iliyopita nimepigiwa simu na kiongozi mmoja wa shule ya seminary kaskazini niende tuongee ikiwezekana nianze kazi huko. Sasa mishahara yao siijui naomba kujuzwa wanalipwaje?
 
wewe unadhania mshahara wa shule za seminari unafanana kwa kila shule...umeambiwa uende mkajadliane na huyo muhusika wa shule yenyewe, sasa wewe unadhani ni majadiliano ya katiba....siyo hivyo kaka ni pamoja na suala la mshahara.
 
wewe unadhania mshahara wa shule za seminari unafanana kwa kila shule...umeambiwa uende mkajadliane na huyo muhusika wa shule yenyewe, sasa wewe unadhani ni majadiliano ya katiba....siyo hivyo kaka ni pamoja na suala la mshahara.
 
seminary gani ya wakatoliki au lutheran, ninachojua mimi Seminari ni charity organization . mishahara yao siyo mikubwa , sema malupulupu ni mengi sana. kama utaishi hapohapo seminary. basi utapewa nyumba, umeme na maji arage ,mayaibure. zawadi nyingi kutoka Jimboni kama vyakula kama michele,mayai na vitu vingine .zawadi nyingi zinatoka wawata, moyo mtakatifu wa Yesu, legio Maria na vikundi vingine makanisani. Seminary ni sehemu pazuri kwa ajila za ualimu.
 
Kaka nenda kapige kazi seminary nyingi kuna maslah sio sawa na za kawambwa
 
inategemea na seminary, nyingine zinalipa vizuri sana, we nenda kamsikilize kwanza.
 
Wakati unasubiri wenzako wako kwenye chakito long way wanaelekea huko. Au unadhani wewe pekee ndo mwl wa fizikia? Nenda maswali hayo utauliza huko huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…