Msaliti hapiganiwi bali anaachwa

prumpeti

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2022
Posts
1,023
Reaction score
2,319
Hili ni jambo ambalo kwa upande wangu nalitizama kwa utofauti kidogo watu wengi wana ingia kwenye matatizo ya kisheria ambayo yanawapelekea mpaka kifungo cha maisha JELA sababu ya usaliti wa mapenzi...

Matukio ya wanaume kuuwa au kujerui watu ambao wana wahisi kwamba wana mahusiano ya mapenzi na wake au wapenzi wao yamekuwepo kwa muda mrefu sasa.

Kitu ambacho kwangu mimi naona ni kosa na kutotumia akili ikifikia mpenzi au mke wako anatoka na kuanzisha mahusiano na mwaume mwingine moja kwa moja huyo afai kuendelea kuwa mke.

Hatua ya kwenda kumshambulia mtu ambae mke wako kwa akili zake amekubali kuivunja nae amri ya sita ni sawa na kukata matawi ya mti na kusubiri kuona umekufa.

Ukitaka kumaliza tatizo tibu chanzo...

Msaliti hapiganiwi msaliti ni wa kutupwa, kuachwa,au hata.............ikibidi

​
 
Wangu nimemwambia, ukienda kugawa, ni yako, wala sitafunwi mimi pale, ni STRAIGHT RED CARD, yaani mie nimdhuru mtu nigungwe jela, ama nijiue kwani nikifa ndio nitakuwa nimeondoka na hiyo mbusus yake, si ndio watakuwa wanajinafasi vizuri kabisa
 
Yani ukiwa unamwagilia moyo na hili jua huku unasoma nyuzi aiseeeee pombe inakolea mpk visigino vinalewa
 
Wangu nimemwambia, ukienda kugawa, ni yako, wala sitafunwi mimi pale, ni STRAIGHT RED CARD, yaani mie nimdhuru mtu nigungwe jela, ama nijiue kwani nikifa ndio nitakuwa nimeondoka na hiyo mbusus yake, si ndio watakuwa wanajinafasi vizuri kabisa
Utaambiwa hujawahi kupenda πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ Ni ujuha yaani kama mtu kakuzingua temana nae kama huwez basi endelea nae mambo ya kuuana tena hayajawahi kuwa na faida.
 
Utaambiwa hujawahi kupenda πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ Ni ujuha yaani kama mtu kakuzingua temana nae kama huwez basi endelea nae mambo ya kuuana tena hayajawahi kuwa na faida.
Kikanuni haswa, kwa mtu anatumia akili zake vyema na si moyo, basi usaliti ni STRAIGHT RED CARD

yaani unaua unaenda jela, mwenzio huku anabaki anakula raha duniani, au ukimuua yeye, bado utaenda teseka jela badala ya kula raha dunianiπŸ˜‚
 
Mwendelezo wa vita ya kumtokomeza msaliti
..

Tukio la kushangaza limetokea katika kijiji cha Borpadaw nchini India baada ya mwanamke mmoja kulazimishwa kumbeba mumewe mabegani na kuzunguka nae mtaani baada ya mwanamke huyo kufumaniwa akiwa na mwanaume mwingine..

Taarifa zinaeleza kwamba mwanamke huyo alitoweka nyumbani takribani wiki moja ambapo badae jitihada za kumtafuta zilianza kufanywa na mumewe pamoja na ndugu zake.

Inaeleza kuwa jitiahada hizo hazikuzaa matunda ndipo mume alipoamua kutoa taarifa police..

Habari zikasambaa kwa kasi na hapo ndipo wasamaria wema walipo mtaarifu mwanaume huyo kwamba mkewe anaishi kinyumba na mwanaume mwingine ambapo mumewe na ndugu zake walienda kwenye nyumba hiyo na kumfumania mwanamke huyo.

Kwa hasira alizo kuwa nazo mwanaume huyo alimpiga na kumvuta nywele kabla ya kuamrisha kumbeba mabegani na kuzunguka nae mitaani huku umati wa watu ukiwafwata wakishangilia...

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…