Watuuuuuuuuuu ni Nguvuuuuuuuuuu
Habari za Kazi Wanajukwaa , Poleni na majukumu ya kutafuta ridhiki kipindi hiki cha serikali ya Mama Samia,Kiukweli KAZI IENDELEE mpaka 2030
Miaka 6 iliyopota ya machozi na damu kwa upande wa CHADEMA tuliona wengi wakifungwa, wakisingiziwa kesi, wakijeruhiwa na hata kupotezwa na kuuwawa, hakuna chama cha upinzani kilichovuja jasho na damu kama CHADEMA, hakuna chama kilichopingwa n ahata kusemwa kinatumiwa na mabeberu kama CHADEMA, CHADEMA iliumizwa vibaya sana na naamini makovu yale hayawezi kufutika mapema.
Wapo walioachwa na vilema vya kudumu, wapo waliopoteza ndugu (baba, mama, watoto, mjomba, shangazi n.k),
Kuna watu/viongozi walikua CHADEMA wakaondoka kwa mbwembwe nyingi wakaondoka kwa kejeli na matusi wakisema CHADEMA imekosa dira, wakaondoka wakitukana mwenyekiti na viongozi wengine wengi wakiamini kabisa watadumu milele huko waendako wakisahau “today’s mine and tomorrow is never promised”
Wengine wakafika mbali sana wakikubaliana na wanayotendewa watu wa CHADEMA wakisema wamezidi ukanjanja
Lahaulaaaa……yakatokea
Leo hii naona wanataka kurudi kundini, naona CHADEMA inawapokea tu, inawatangaza (INADHANI SIFA SIJUI)
Mwingine Juzi amerudi anasema, “Hajarudi na V8 amerudi na pengo” sasa tumsaidiaje sisi, juzi wa Serengeti nae anaomba kurudi, yule si ndio aliondoka kwa kejeli na watakuja wengi sana kwasababu wenye chama chao waliokipigania kwa mjasho na damu wamerudi (baba zao hawakulala, hawakula, walikesha wakipigania chama chao)
Haiwezekani wao watake raha tu wasitake shida
CHADEMA hata Yesu mwenyewe alisema Ingekua heri msaliti asingezaliwa.