Msaidizi wa IGP, Gerald Ryoba, mkewe, watoto wawili na wengine wawili wafariki kwa kusombwa na maji

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
10157292_1018804184844447_3899799815930489279_n.jpg

Ryoba.png

Afande G. RYOBA akiwa safarini na mkewe kuelekea Dar. Gari yao ilisombwa na maji na mpaka sasa imepatikana miili ya mkewe na mtoto lakini mwili wa Insp. RYOBA mpaka sasa bado haujapatikana.

Timu ya wapelelezi imekwenda eneo la tukio huko Kibaigwa kwa hatua zaidi.

================

WATU 8 wamefariki dunia katika ajali iliyosababishwa na gari kusombwa na maji huku watu 6 wakiwa wa familia moja.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Davidi Misime amesema majira ya saa tatu usiku Jumapili, wananchi wa Kibaigwa walitoa taarifa jeshi la polisi kwa madai kwamba kuna gari limesombwa na maji na limetumbukia katika mkondo wa maji.

Amesema baada ya jeshi kupata taarifa hizo polisi walijitahidi kutoa gari hilo aina ya Rav4 yenye namba za usajili T516 DEP na kubaini kwamba jumla ya watu sita wa familia moja wamepoteza maisha katika familia moja.

Misime amewataja waliofariki kuwa ni Msaidizi wa Inspekta wa Jeshi la Polisi (IGP) Gerld Ryoba, mke wake Fidea Kihondo, watoto wawili binti wa kazi, na Koplo Ramadhani ambaye ndiye alikuwa anaendesha gari hilo.

Amesema wana familia hao ilikuwa ikitokea rikizo mkoani Geita na walikuwa wakirejea kazini Dar Es Salaam.

Amesema ajari hiyo ilitokea maeneo ya Kibaigwa bwawani kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo ya Njoge, Embaemba, Kiteto na bonde la Ndurugumi.

Misime amesema gari hiyo ilikuwa limeharibika sana na walilazimika kulikata gari hilo na kuwakuta watu wanne ndani ya gari huku wawili wakiwa nje ya gari ndani ya maji.

Hata hivyo Misime amewataja watu wengine wawili wanaume ambao walikutwa katika maji.

Kati ya watu hao wawili ambao ni wanaume amemtaja afisa mifugo kata ya Pandambili na anafahamika kwa jina moja la Ludege.

Amesema mmoja mpaka sasa hajatambuliwa kwa jina huku madaktari wanafanya utaratibu wa kuandaa miili kwa ajili ya kuwasafirisha.

Amesema mtoto wa kazi aliyefamika kwa jina la Saraha atapelekwa Mbinga, Koplo Ramadhani anapelekwa Lindi huku miili ya watu wanne inapelekwa Geita.
 
Last edited by a moderator:
Kibaigwa Dodoma???ndipo aliposombwa au ndio gari na maiti zimepatikana???
 
image.jpeg
View attachment 314805
Afande G. RYOBA akiwa safarini na mkewe kuelekea Dar. Gari yao ilisombwa na maji na mpaka sasa imepatikana miili ya mkewe na mtoto lakini mwili wa Insp. RYOBA mpaka sasa bado haujapatikana.

Timu ya wapelelezi imekwenda eneo la tukio huko Kibaigwa kwa hatua zaidi.
Kama tukio hilo la mafuriko limetokea pale kabla tu ya Kibaigwa(km 1 au 2 kutokea DSM), watu wengi hawaelewi, pale wakati wa mvua ni mahali hatari sana.
Wengi wamepotea pale kwa mwendo kasi wa maji.
 
pole sana wafiwa, Mwenyezi mungu awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu
 
Mkuu kulikuwa na watu wangapi kwenye hilo gari? na vipi kuhusu hao wengine?
 
Pole sana kwa wafiwa, kifo kibaya sana hiki gari imekuwa kama srepa ya miaka ya 80!
 
Pole sana kwa wafiwa, kifo kibaya sana hiki gari imekuwa kama srepa ya miaka ya 80!
Inaogopesha sana. Yaani nimejikuta narudi juu kuangalia tena na tena hilo gari. Mungu awapumzishe mahala pema
 
Back
Top Bottom