Msafara wa Viongozi wa BAVICHA Wazuiwa na Polisi Kilimanjaro

Msafara wa Viongozi wa BAVICHA Wazuiwa na Polisi Kilimanjaro

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235

TAARIFA KWA UMMA​


Msafara wa viongozi wa BAVICHA Taifa na Kanda ya Kaskazini, ukiwa njiani kuelekea nyumbani kwa familia ya akina SOKA kama sehemu ya kuenzi mashujaa wetu, umekumbwa na vizuizi visivyo halali. Magari ya polisi yamezuia msafara huo takribani mita 100 kutoka barabara ya Kibosho, mkoani Kilimanjaro.

Ni dhahiri kuwa hatua hii haikuwa ukaguzi wa kawaida, bali ni dhamira mahsusi ya kuzuia msafara kuendelea na shughuli zake kwa amani. Idadi ya magari ya polisi imekuendelea kuongezeka eneo la tukio, jambo linalozaa hofu na kuashiria nia ya kuchochea vurugu na kuvunja amani badala ya kuilinda.

Tunalishii Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kuacha mara moja vitendo vya uchochezi na matumizi mabaya ya nguvu. Wajibu wa msingi wa polisi ni kulinda usalama na amani ya raia wote bila upendeleo.

CHADEMA hatutatisishwa wala kukatishwa tamaa na mbinu ovu za kuzuia harakati halali za kidemokrasia. Tutaendelea kufuatilia kwa karibu hatua zote zinazochukuliwa, na tutasimama imara katika kulinda haki, amani na demokrasia nchini mwetu.

snapins-ai_3715691776356508522.jpg
snapins-ai_3715691776339680289.jpg
 
Back
Top Bottom