Huitwa Afisa Mazingira (Environmental Officer) mara nyingi kazi zao huwa ni kuchunguza miradi(mfano. Viwandani,migodini,shughuli za ujenzi n.k) au matukio yanayoweza kuleta athari kwa viumbe hai na visivyo hai. Pia kutafuta njia mbadala za kupunguza au kuondoa hizo athari. Kuhakikisha wafanyakazi wanafanya kazi katika mazingira safi na salama na kuwashauri watu juu ya umuhimu wa kuhifadhi na kutunza mazingira. Ajira zao huwa zipo serikalini na mashirika binafsi.