Wanaokuvunja moyo hawajui wanachokiongea humu....
Inawezekana kabisa ukaanzia level ya "Certificate" fani yoyote kwa kutumia CSEE results. Pili unaweza kuanzia level ya "Diploma" fani yoyote ukitumia sifa ya "ACSEE" ilimradi tu uwe na vigezo vya ufaulu...
Mimi mwenyewe nina fani 3 tofauti, mbili nina Advance Diploma kwa mbinu hiyo hapo juu na moja level ya Masters. Hii ya Masters niliianzia level ya Diploma kwa kutumia sifa ya ACSEE wakati nikiwa kazini na professional nyingine. Na ndiyo ninayoipenda mno na kuiniingizia kipato kizuri kwani imenipa mwanya mkubwa wa kufanya kazi binafsi baada ya muda wa ofisi.