Ungetuambia Model ya hiyo Desktop na manufacture ya hiyo Bios labda kama ni AMI, Phoenex n.k maana kila model ina njia tofauti za kureset bios password.
Labda jaribu hizi njia,
1. Chomoa cmos battery then
irudishie ila hii ni kwa bios za
zamani sana,
2. Angalia pembeni ya Cmos battery kama kuna jumper, kama ipo chomoa mguu mmoja weka kwa mwingine.
3. Tumia njia ya mlongo wa nyuma (backdoor password) kila manufacture ya Bios wana master password incase kama mtu amesahau password. Ingia google e.g AMI backdoor password.
4. Short-circuit au discharge Bios chip, hii njia ni kwa modern computers ambazo hazihifadhi kumbukumbu za bios kwenye Cmos battery. Ila hii njia ni kwa wataalamu wa umeme wa motherboard kwa sisi wengine tutaua circuit.