Habari wanajamvi,
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 26.Miaka minne iliyopita nilikuwa na boyfriend ambae nilimpenda sana lakini kwa bahati mbaya katika safari yetu ya mapenzi ilidhihirika wazi kuwa hakuwa na mapenzi ya dhati kwangu kwa sababu nilikuja kugundua ana msichana mwingine.Kwa kifupi alinisumbua sana hadi ikafikia kipindi akaniambia nimpe space maana anaona kama ananiumiza na hawezi kumuacha huyo msichana mwingine.Niliumia sana,nikawa najaribu kumove on lakini nikawa nashindwa kwa sababu bado nilikuwa nampenda.
Baada ya muda kupita nikakutana na mwanaume mwingine,alikuwa ni mtanashati na mwenye tabia njema tu,kijana huyu niliwahi kusoma naye sekondari ila yeye alinizidi kidato kimoja mbele.Nadhani kutokana na upweke niliokuwa nao nilijikuta naanzisha naye mahusiano na kidogo kidogo nilianza kumpenda ingawa mawazo ya yule wa mwanzo yalikuwa hayajaniisha bado.Katikati ya mahusiano haya mapya niligundua pia huyu mwenzangu yuko katika mahusiano na msichana mwingine.Kwa jinsi nilivyokuwa na stress,sikutaka hata kumuuliza kwani nilijiona sikufanya jambo la kunipa afadhali bali kuniendelezea maumivu yaliyopita.Kwa hiyo nikaanza kumuacha kimyakimya kwa kupunguza mapenzi na mawasiliano pia ili niweze kutulia na kuweza kuanza upya.
Wakati napitia hayo yule boyfriend wa mwanzo alirudi kwangu akionyesha kujutia makosa yake,aniomba msamaha na kuahidi kwenda kujitambulisha kwetu tayari kwa kufunga ndoa.Sijui ni kwa ajili nilimpenda sana au umburula wangu nikajikuta nimemsamehe na kurudisha mapenzi kama mwanzo,huku nikitafuta sababu ya kumwacha yule mwanaume mwingine.Kiukweli nilimtafutia kila sababu ya kumwacha lakini ilishindikana kwani naye alibadilika akaonyesha mapenzi kwangu sana na akawa mkweli kuhusu mahusiano aliyokuwa nayo kwamba ni girlfriend wake ambaye hakuwa happy katika mahusiano yao ndiyo maana aliamua kuwa na mimi na kwa sasa amaeamua kumwacha kabisa ili awe na mimi.Kiukweli nikijikuta katika dilemma kubwa sana.
Nilishirikisha Mungu katika hili kwani nilijikuta nachoka kudate nao wawili kwa wakati mmoja (hata sijui kwa nini nilikuwa sikamatwi).Ninakiri kwamba nilichokuwa nafanya si kizuri ila nimeamua kuwa muwazi ili niweze kusaidiwa.Baada ya mwaka na nusu nikiwa katika hali hiyo,nilikuja kugundua huyu boyfriend wa mwanzo niliyemsamehe yuko kwenye mahusiano na mwanamke mwingine na wapo kwenye mchakato wa kufunga ndoa.Nilipomuuliza alinijibu wazi kuwa ni kweli na tuachane mazima.Niliumia na kulia sana,na ilinichukua muda mrefu kurecover ila mwisho wa siku ilinibidi nikubaliane na ukweli na maisha yaendelee.Nikabaki na huyu kaka ambaye kiukweli mapenzi yake kwangu hayajawahi kupungua,sasa mimi nikawa natumia efforts nyingi kumpenda.Cha kushangaza ni kwamba kadiri siku zinavyokwenda mapenzi yangu kwake ndo yanazidi kupungua.Ni karibu mwaka sasa sijielewi kabisa,sina feelings naye kabisa na yeye hata halioni hilo badala yake yeye kila kukicha ndio anazidihsa mapenzi kwangu.
Sasa ndugu zangu,kilichonileta kwenu ni kuomba ushauri na kujua kama kuna mwenye experince na hii scenario.Je nimwache niendelee na maisha yangu?Au niendelee naye labda kuna siku moyo wangu utafunguka kwake?Ananipenda na anataka kwenda kwetu kujitambulisha,lakini ndi hivyo hata sex si enjoy mpaka siku nyingine nasingia naumwa mradi tu nisikutane naye.Ungekuwa wewe ni mimi ungeendelea naye?Au hii imetokana na yule niliyempenda akanitenda?(ANGALIZO:HUYU NI RAFIKI YANGU ANAOMBA USHAURI).