Wadau naanzisha Uzi huu kwa madhumuni ya kupata msaada. Mini Huawei Y530....nilifanikiwa kui-root... Nikafanikiwa bila wasiwasi..na nikafanikiwa kutumia faida ya Ku root kwa kung'oa bloatware.... ... Nimefurahi kiasi... Lengo ni nyie wadau mnisaidie jinsi ya kupata custom ROM ya Huawei Ascend Y530. Kutoka 4.3(jelly bean ) mpaka KitKat.... .. Nime Google.. Nime bing. Nimezurura sana. Ila naambulia maelezo yasiyoeleweka. Na kuambulia broken link... Nimeingia XDA forum.. Naona Giza.
Ninaomba mnisaidie kwa hili...
S/O kwa Fareal kwa msaada wako . ila nahitaji maelezo zaidi.
WADAU KARIBUNI....... NISAIDIENI KWA HILI
mkuu, hii simu mpaka sasa kuna custom rom ambayo iko based on CyanogenMod, ila haijakamilika, kama we ni mpekuzi kuna uzi XDA utauona unazungumzia development za hii simu,
ambacho kipo ni custom roms ambazo ni clockworkmod backups based on ile default emui rom ambayo inakuja na simu...
mfano kwenye hizi cwm rom, inakuwa ni ile default rom ila imeondolewa launcher ya huawei na inawekewa rom ingine, pia apps za google zinaondolewa inabaki playstore, pia inaongezewa uwezo wa livewallpapers, na vitu vingine, uzuri wake izi uwa ni light sana. so utasave space yako nyingi