Mpige injili akishaokoka pombe kwa heri na kuwajibika ataanza........huko ndo kuvumiliana katika shida na raha.
mvumilie mpe muda wa mabadiliko kulea watoto peke yako tena matineja kuna changamoto nyingi sana usisubiri akutoe out one day panga wewe trip may be hata ya zanzibar mkaongee kwa kina natumaini suluhisho litapatikana tu kati yenu
Mimi ni mwanamke nina miaka 37 sasa hivi,nimeolewa na nina watoto watatu miaka 17,13 & 6yrs.Nimeishi na mume wangu kwa miaka 18 sasa hivi,mume wangu ni maasai wa mjini sio wale wavaa lubega.
Tatizo ni huyu baba nimembeba sana mpaka naona nimechoka na vile umri umeenda sijui nifanyeje. Sio mwanaume muwajibikaji kabisa.
Hajui ada za wattoo zinatoka wapi, chakula, maendeleo ndani ya nyumba, hajui chochote yeye ni kama mtallii.Hata akiona pazia liko upande hatengenezi au chumba hakina bulb hajigusi, ni mimi ndio nifanye.
Ada za watoto ndio kabisa akijatahidi sana kama ada ni laki 4 basi atatoa laki 2 tena kwa shida na kwa awamu. Akikuta hela zako au pochi umeweka vibaya anaruka mpaka na hela zako.
Sio muwajibakaji hata tone yeye ni starehe na starehe na yeye.
Kweli nimevumilia sana tokea mwanzo ila mbona naona kama siwezi tena? mzigo umenilemea na hana msaada wewe ndio ukimbizane watoto watakula nini, watasomaje, watavaa nini, nyumba inaitaji nini etc.
Ndoa ni kwa shida na raha,nimejenga nyumba mwenywe na kila kitu nimefanya mwenywe tena yeye ulikuwa ukimpa hela ndio anaenda kulewa, mpaka leo ana miaka 43 sasa hivi ni wa kurudi usiku wa manane.
Nimechoka kuvumilia jamani namuambia aondoke aniache maana nyumba ni ya watoto na ni nguvu yangu, mwenywe hataki.
Ukipika chakula akikuta anakula hajui hata kinatoka wapi.
Juhudi zote za maendeleo na watoto ni mimi mwenywe.
Haya maisha yamenichosha sana jamani nifanyeje nimejikuta simpendi tena kabisa na sina hamu nae kabisa hata ya mapenzi.
Sina mpenzi wa nje basi tu nimeona huu ni mzigo ambao umefika mwisho,nataka nimuche nafanyaje na yeye ndio amekataa kutoka ndani ya nyumba kabisa? nimechoka kweli kwei.
Toka kanioa ni ile miezi ya awali ndio alishawahi nitoa out,sikumbuki hata mara ya lmwisho aliniambia mke wangu twende out ni lini, au tukakaa kupanga maisha/maendeleo ya watoto au chochote ni lini.
Mimi ndio wa kukimbizana na maendeleo ya shule ya watoto. Kila siku ni kuomba kulipa ada kwa instalment.
Nimekua ndio kama niko peke yangu yeye akija usiku na mtungi wake ni kelele na kulala.
Yuko kama vile anaishi guest,akija usiku saa zingine fujo na kelele. Sikumbuki hata mara ya mwisho ameshawahi nipa laki ya matumizi au hata elfu 50 ni lini? akitoa hela ya chakula ni elfu 20 kama mara ya mwisho kanipa miezi 2 iliyopita.
Hata nikiwa na msiba kwetu hakanyagi wala haudhurii.
Jamani hebu nishaurini nifanyeje?
Himidini nashukuru sana na wote mliochangia mada. ni kweli inaonekana nimelea mm hili tatizo ila ni sababu i wanted the best for our kids and our home. mimi ni mwanamke wa kihaya nisiokubali umaskini hata kdg ndani kwangu. napigana na kufanya kazi kwa bidii sana. nimeshawashilikiza wazazi wa pande zote mbili na hata wazamini wa ndoa. wote wanalijua hilo na wanamjua fika kijana wao ni wa namna gani. he is a kind of ignorance he dont care hurting you at all....unyumba wenyewe naweza hata kaa mwezi hatujagusana. sababu kila mara anarudi usiku wa manane. ni mfanya bishara its not easy to control his income. nadhani ni mila ndio zinamsumbua i really dont know. yaani wapendwa nimechoka mpaka bac. nimevumilia mpaka sasa hv nina vidonda vya tumbo na pressure ya kushuka. nawaa bila majibu.nifanyeje sijui. ndio maana nikaona nililete hapa kwenu. returning the love back is not easy coz i just dnt love him anymore kwa yale yote anayonifanyia.
Pole sana dada kokuemage
Mi nadhani uongee na hao friends wake ... kuna watu hawana msimamo wao ni rahisi sana kufata influence ya friends
sasa kama jamaa yeye ni pombe tu ... am sure he doesnt go out peke yake.
kama hapatikani usiku basi make time ya kuongea nae kila siku asubuhi during breakfast kabla hajapiga mitungi
Na Siku zote tunavumiliwa sisi wanaume tu?!Mpige injili akishaokoka pombe kwa heri na kuwajibika ataanza........huko ndo kuvumiliana katika shida na raha.
Thanks Sita ila ni ngumu coz yeye anarudi mmeshalala kuamka mimi nimeajiriwa lazima saa 12 niwe macho kwa ajili ya kwenda kazini yeye ndio kwanza anakoroma anakusubiria ukishaondoka ndio aamke. mara chache sana tunawa wote nyumbani. nimeshaongea nae sana mpaka na marafiki zake wote wanasikitika hivo hivo ila habadiliki sijui kwa nn. Watu8 ni kweli never marry a man expecting him to change. hii na iwe fundisho kwa watu wote ambao hawajoa/kuolewa. Nadhani na yeye hana msimamo pia.
umesema vema ndugu, huyo mpige Injili na kumwombea tena maombi ya kuatamia. Mungu ni mwema atamfungua ktk hivyo vifungo vya mwovu vya pombe. Kumwacha hiyo sio tiba nzuri kabisa na kamwe isitumike. Imeandikwa ''ndoa na iheshimiwe na watu wote'', pia imeandikwa ''alilo liunganisha Mungu mwanadamu asilitenganishe''. Mpende baba watoto wako, fanya toba kwa ajili yake, Mungu hatakutupa hilo ni jaribu tu.
Na Siku zote tunavumiliwa sisi wanaume tu?!