Habar wanajamvi
Natumai ni wazima na buheri wa afya. Niende kweny mada husika.
Nina msichana ambaye Niko nae kweny mahusiano kwa zaid mwaka na nusu sasa, kiufupi ni kwamba bado Niko nae na ananiheshimu na kunithamin sana japo hali ndo hio ya Jiwe..
Kiufupi wasifu wake ni mchaga wa Uru.
Dhamira yangu ni kuanza nae maisha kama mke na mume endapo Mungu ataendelea kutuonesha upendo huu.
Kama mjuavyo kwa hili kabila maranyingi hukosi pingamizi za hapa na pale.. Ila kwangu sio issue sana.
Sasa katika harakati zangu za kiume kama mwez mmoja hivi ulopita nikakutana na msichana mwingne... Nikaanzisha mawasiliano nae so, kukawa na chatting za hapa na pale bahati mbaya mtt wa watu kanogewa kanifungukia...
Labda niseme kitu kutoka ndani ya nafsi yangu jins nilivyo, ni mpole sana na sipendi kupindisha ahadi niloiweka kwa mtu. Nakua na huruma sana na mtu, tofaut na ninavyojijali mwenyewe.
Sasa nae huyu binti ananiletea swaga za kuishi pamoja na kuanza maisha. Na amefika mbali zaid kunitambulisha had kwa wazaz wake, kitu ambacho sikutegemea na had wazaz wakaniita nikawasalimu, na Mimi kwa heshima ya wazazi nikaitikia wito, tukasalimiana.
Kitu ambacho kinanitesa hapa ni jinsi ya kujitoa kwa huyu binti wa pili, bila kuumiza nafsi yake kwan kila nikifikiria mipango nilopanga na huyu mchga wangu na sipend kuitelekeza, napata kigugumizi. Sipend kumuumiza kihisia sabab sipend kuona mtu anateseka kwa ajil yangu.
Na huyu mchga nikitania tu kusema ile tuachane ni pressure na kuumwa siku nzima.
Labda mnipe ushauri wanajamvi ni njia gan sahihi, ya kujikwamua hapa. Kinachonipa Mawazo zaid ni kwamba huyu mchaga nilimtafutia kazi mahali, na mwezi ujao ndo anakuja, so najua kutakua na mizengwe ya hapa na pale sabab ni mfuatiliaji sana na huwa sipend kujificha kweny chatting zangu so atagundua tu. Najua kwa umri wetu huu 25s...ni wachache wanaofikia zaidi ya miaka mitatu, wakiwa pamoja.
Nisaidieni nitoke kweny mawazo haya... Au wapi nilikosea au kipi nikifanye ambacho sitamuumiza mtu.
Best Regards