Ngoja nikupe heads up mbili tatu.
Lazima ujue kua hiyo research proposal ndiyo utaifanyia research hivyo usiifanye kua pana sana naamini hiyo title supervisor wako hajaipitisha au kama kaipitisha anataka kukukomoa.
Ukisema secondary schools, Tanzania kuna secondary schools ngapi? Utazunguka ngapi? Utajikuta una kitu kikubwa mno ambacho utashindwa kukihimili. Hivyo angalau ungeandika hiyo title na kumaliza na 'Case Study of Chamwino District' 'Case Study of .....'
Pia endelea kupunguza upana wa title kwa kuonyesha kua ama utadeal na shule za serikali au za binafsi. Ukiacha hiyo title kama ilivyo maan yake utatakiwa kuonyesha shule zote za Tanzania. Halafu siku ya kufanya research utazunguka Tanzania nzima katika shule zote.
Kwahiyo ningekua wewe pengine title yangu ingekua hivi 'Factors Affecting Performance in Geography Subject in Government's Secondary Schools: Case Study of Magomeni Mikumi'
Au eneo lolote unalohisi utacover kwa urahisi. Pia vyuo hutoa guide ya jinsi wanavyotaka Research Proposal zao ziweje, nenda uliza kwa Supervisor wako au mkuu wako wa idara. Ningetafuta yangu na kukupigia picha uisome ila itakua ni kujiexpose.
La mwisho: Hakuna raha kama kuifanya research yako mwenyewe unakua comfortable na confidence ipo juu. Pia usiwe mvivu kudeal na supervisor wako, usinune chochote atakachosema fanya.
La mwisho tena; WanaJF acheni majibu shitty, mtu kama hadi kaandika uzi ni ama umpe msaada au upige kimya.