Hakikwanza
JF-Expert Member
- Dec 11, 2010
- 4,035
- 1,003
Habari za kazi ndugu. Jamani tunaomba msaada wenu watanzania juu ya jambo hili gumu sana. Nina ndugu yangu kila akipata mtoto yeye na mke wake, watoto wanakufa baada ya kuzaliwa. Wanapozaliwa tu joto hupanda sana na baadae hupelekea kufa. Hivyo mpaka sasa hawana mtoto inasikitisha sana. Watoto wawili wameshatangulia mbele ya haki. Vipimo vyao vya damu ni
Mama ana kundi "O" la damu na RH positive
Baba ana kundi "A" la damu na RH negative
Tunaomba ushauri wenu wataalamu wa afya je kunaweza kuwa na shida kwenye huo muunganiko wa hayo makundi ya damu? Tunaomba msaada wenu wa kitabibu. Mwenyezi Mungu awabariki natanguliza shukrani zangu za dhati