Ndg zangu nawasalimu wote amani iwe kwenu!
Naomba kupewa ushauri wa kisheria kwa jambo kama hili, mfano kama baba na mama wamepata mtoto na ili kuzuia kupata mtoto mwingine ndani ya muda mfupi wakaamua kwenda hospitalini/ dispensary au kituo cha afya kutaka ushauri na kisha kupewa ushauri na mtaalamu kama nesi au doctor kutumia njia za kisasa kupanga uzazi. Wahusika yaani baba na mama wakakubali na mke kuwekewa KITANZI lakini katika uwekaji yule mhusika akakosea kukiweka yaani akaweka vibaya huku mteja akiamini amewekewa njia madhubuti ya kuzuia kupata mimba nyingine ya haraka, kisha ndani ya muda mfupi mhusika anagundua ana mimba nyingine baada ya dalili za hapa na pale na klsha kuthibitisha kwa kupima na kugundua kwamba kweli mimba ipo. Mteja aliporudi kujua imekuwaje kapata ujauzito wakati aliwekewa kitanzi na bado kipo ndani na tena kiliwekwa na mtu aliayeaminiwa kwenye kazi hiyo, dokta katika kuchunguza akagundua kwamba nurse alikosea kukiweka hali liyoplekea mhusika kupata ujauzito nje ya muda aliotaka yeye.
Katika mazingira kama haya mhusika anakuwa ameathirika kwa mengi kwanza kuwa na ujauzito katika muda ambao hakupanga, kuwa na ujauzito mtoto wa awali angali bado ni mdogo sana, kuharibu ratiba za kikazi na kimalezi za wahusika, kuathirika kisaikolojia na kiuchumi na wakati mwingine kuonekana mtu wa ajabu mbele za jamii. Sasa je katika mazingira haya nini haki ya muathirika ? je ana uwezo wa kufungua mashtaka dhidi ya mtaalamu au hospitali husika? . Najua mambo kama haya ya kufungua kesi kwa mazingira kama haya ni mageni katika nchi yetu lakini je kisheria muathirika ana haki?
Ushauri wenu ni muhimu ili kuongeza uelewa na kutatua changamoto hii.
Nawasilisha
Bringbackbrothermoalive.