Ndugu zangu poleni na majumkumu, nipo namfanyia mdogo wangu application ya NACTE (certificate), nimezowea kupitia vyuo kadhaa kabla ya kusave CHOICE, naangalia slot na fee ya chuo nakuwa nanote kwenye karatasi baadae natulia na kufanya CHOICE, muujiza ulionitokea jana usiku, wakati nikiendelea kupitiapitia chuo ghafla mtandao ukakata, nilipojarifu kuanza upya nikakuta tayari dogo kajaziwa 3 CHOICES kati ya vile vyuo nilivyokuwa napitia pitia, kiukweli sikusave CHOICES na vyuo alivyojaziwa si mimi wala yeye hakuna anaevitaka, kibaya zaidi course aliyojaziwa kama first choise haitaki kabisa. Nikapata wazo la kuchange choices hicho kipengele hakipo, kipengele cha kufuta choices nacho hakipo, nimejaribu kupiga cm za NACTE zilizoandikwa chini zote hazipatikani, nisaidieni waungwana maana mimi na mdogo wangu wote tumechanganyikiwa, nitawezaje kufuta hizo choices na kuadd tunazozitaka sisi?