Mimi nina mpenzi wangu ambaye tumekuwa naye kwenye mahusiano takriban miezi sita sasa, nimesafiri kikazi nje ya mkoa tulipokuwa tunaishi ingawa yeye alikuwa anakaa kwa wazazi wake huku mimi nikiishi mwenyewe kwenye nyumba niliyopanga, imepita miezi miwili sasa hatujaonana kimwili nae, huwa tunawasiliana tu kwa simu! Katika kuchati kwetu majuzi nikamuuliza ni changamoto gani anazokutana nazo nikiwa mbali nae? Alinijibu kuwa kuna rafiki zake ambao alisoma nao O-level wanamsumbua, yaani wanamtaka kimapenzi! nilichomjibu ni kwamba unawaonaje hao jamaa, unawapenda?? Akaniambia hawapendi na ameshawaambia waachane nae na kasema hapokei simu zao! Nina wasiwasi sana mpenzi wangu anaweza kubadili msimamo wake na kuwakubalia hawa jamaa,. Naombeni msaada wenu jamani maana nampenda sana mpenzi wangu na sitaki awe na mtu mwingine.