Natoka safarini Dar naelekea Tanga nikiwa na rafiki yangu jina anaitwa Maalim(Si jina halisi),
katikati ya safari gari inasimama nashuka,
Wakati huo maalim hakushuka! nikiwa narudi kwenye basi ghafla nakutana na dada(Ana asili ya kiarabu) ananizuiya kupanda hiyo gari!,
Basi naamua kuachana na hiyo gari! natembea kwa miguu,
Njiani nakutana na dada flani ni kama nimewahi kumuona sehemu ila simkumbuki,
Namsalimia ila hataki kuitikia hivyo naachana nae!
Kichwani analo beseni nadhani lilikuwa na matunda anaonekana kama ni mjasiriamali wa matunda,
Ghafla nakumbuka nilikua safarini na gari imeniacha! hapo naghafirika kidogo
Natembea kidogo nakutana na mti nadhani ni wa mwembe!
Chini yake nakuta pesa nyingi hivyo naanza kuziokota,
Baada ya hapo natoka hilo eneo naenda eneo jingine,
Huko nakutana na rafiki zangu mbali mbali naanza kuwagawia zile pesa nilizookota!
Nafanya hivyo huku nikiona hizo pesa hazitanifaa kitu kwa kuwa siko safarini tena nawapatia zotee,
Katika hali ya kustaajabisha namkuta yule dada niliyemsalimia akagoma kuitikia salamu naye alikuwa katika kundi la wale rafiki zangu,
Papo hapo na rafiki yangu Maalim(Si jina halisi) anakuja na kunilaumu kwanini sikuwa pamoja naye safarini,
Najaribu kujitetea kuwa nilizuiliwa na dada mmoja ambaye simfahamu! ila ni kama Maalim haniamin anasema yeye ameenda na kurudi siku hiyo hiyo ila mimi nimeshindwa kwenda kwa nini(Kumbuka tulikuwa tukielekea Tanga).
MWISHO, HICHI NI KISA CHA KWELI AMBACHO KIMENITOKEA KWENYE NDOTO, USIKU WA KUAMKIA TAREHE 30/01/2019,
BADO NATAFUTA MAANA YA NDOTO HII.
Sent using
Jamii Forums mobile app