Naomba nipewe ujanja / mbinu ya ama kumuomba namba ya Simu Mwanamke mkiwa katika Daladala lililojaa bila kuona aibu au ile ya kumpa Mwanamke namba yako ya Simu ' kimya kimya ' bila ya kuathiri masikio au macho ya Abiria wengi wa Daladala ambao wengi wao huwa na Wivu / Husuda halafu pia wana Visununu / Visirani mno kwa Wenzao ambao hufanikisha mambo yao ndani ya huo Usafiri.
Nijibuni upesi hizi mbinu tafadhali ili hili zoezi nilianze rasmi mapema tu Kesho asubuhi kwani mazingira yangu mengi ya ni Daladala hivyo nahisi nami huko naweza kuopoa Kitu cha maana au basi nami naweza kila Siku nikawa navua tu ' Samaki ' ndani ya hizo Daladala.
Natanguliza Shukran Kwenu nyote.
Nawasilisha.