Wakuu Tume ya ajira wametoa tangazo la kazi, lakini kinachonishangaza katika maelezo ya jumla wamesema TRANSCRIPT hazitakubaliwa. Tume ya ajira wamekuwa wakichukua na kukubali maombi kwa transcript walichokuwa wanakikataa ni ile parcial transcript. Je wakuu hii imekaaje? wenye ufahamu na hili tafadhali wakuu.
"Transcripts", "Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
Wanasema watu waliowajiiri kushotlist hawakuzingatia kigezo cha cheti, wao walikuwa wanaangalia ufaulu. Kwa maelezo yao ni kwamba walikosea kunishotlist.
Ila kuna rafiki yangu alishawahi pata ajira kupitia hao hao utumishi, hakua na cheti wala transcript. alikua na provisional results tu. kama ipo ipo tu, msichoke wazee kuapply.