Access ni database hii inakuruhusu kuhifadhi data kutengeneza relationships baina ya data hizo na ku query hizo data.
Kwa mfano unaweza ukawa na table ya Mkoa, Shule na Wanafunzi kila mwanafunzi awe na relationship na shule fulani na kila shule iwe na relationship na mkoa fulani.
Unaweza ukaenforce hizo relationship kwa mfano hauwezi kumwingiza mwanafunzi kwenye table ya Wanafunzi bila kumpa shule ambayo iko kwenye table ya Shule na unaweza kutengeneza data entry forms za kuwezesha mtu kucapture hizo data kulingana na hizo relationships.
Kisha unaweza ku query hizo data kwa mfano ikupe wanafunzi wote wa shule fulani, au wanafunzi wote ambao wapo kwenye mikoa inayoanzia na herufi D etc. Pia Access ina uwezo wa kutumika na multiple users wakaaccess same file kwa wakati huo huo.
Excel ni spreadsheet madhumuni yake makuu ni kuhifadhi data hasa namba katika muundo wa worksheet za karatasi zinazotumikaga na wahasibu, kisha kuzifanyia calculations mbalimbali na kuchora graphs ili kuweza kuielewa data vizuri zaidi.
Ila kutokana na urahisi wa matumizi ya Excel huwa inatumika kwa kila kitu siku hizi, ikiwemo kazi ambazo singefaa zaidi kwenye Access.