Msaada tafadhali

JATELO1

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2011
Posts
1,230
Reaction score
307
WANAJF;
Ndugu zangu nina ndugu yangu alipata division 4 ya point 29 baada ya kusoma QT kwa miaka 2. Matokeo ya masomo kama ifuatavyo, History C, Kiswahili D, Civics D, Geography D, English Language D, English Literature F, na Maths F. Na kabla ya hapo alifanya Course ya Mechanics na Udereva kwa mwaka moja na kuhitimu kwa daraja B pale chuo cha Future World Driving College Buguruni Dar es Salaam.

Bwana mdogo alikuwa na mpango wa kwenda kufanya Ualimu Grade A, hivyo alilazimika kureseat mwaka jana (2012) ili apate credit ya kumuwezesha kujiunga Chuo cha Ualimu. Lakini mwaka huu kukawa na tangazo kutoka Wizarani kwamba, kozi ya ualimu wataaruhusiwa kufanya wale waliofanya mtihani mara moja na kupata matokeo yanayowawezesha kujiunga na Chuo cha Ualimu. Na kwa msingi huo, bwana mdogo itakuwa vigumu kupata nafasi, kwani yeye hana matokeo mazuri kwa mara moja kama hitaji la nafasi za Chuo cha Ualimu.

Sasa naomba ushauri kuhusu namna nitakavoweza kumsaidia huyu bwana mdogo katika mambo yafuatayo, kwani naona kama anataka kuchanganyikiwa kwasababu kwasasa ana miaka kama 28, na mimi kwasasa nipo mbali, lkn nahitaji sana kumsaidia katika Career path.

1. Je kwa matokeo hayo ya Sekondari na hayo matokeo ya chuo cha Mechanical, bwana mdogo akiomba nafasi ya kufanya course ya Mechanical VETA ataweza kuchaguliwa? Hii ni kwasababu, tayari ana uelewa na umechanical na udereva. Alitaka asome NIT lkn ilishindikana, kwani hakufanya Physics na pia alifeli Maths. Kwahiyo naomba kwa mtu yeyote mwenye uelewa anisaidia kuhusu uwezekano wa kujiunga VETA kwa matokeo hayo.

2. Je, kama mtu akisoma kwenye Vyuo vya Maendeleo ya Kijamii (Community Development Institute) kama Bohare Musoma au Kilolo Iringa, Je watu wanaopitia hivi vyuo wanafanya kazi maeneo gani? nauliza hivi kwasababu nimejaribu kufuatilia kwenye website zao lkn sijapata kuona hata aina ya kozi zinazofanywa pale na kuweza kunipa picha ya hatima ya wahitimu kwenye vyuo hivi vya maendeleo ya jamii. Naomba mwenye uelewa katika hili anisaidie wazo tafadhali.

3. Wazo lolote linaloweza kusaidia ili huyu bwana mdogo aweze kuwa na future.

Natanguliza shukrani.
 
vipo vyuo vingi tu ila namshauri aende veta dar na vyet vyake atapata pa kuanzia.mtoto wa kiume anakomaa mwenyewe hadi kitaeleweka tu mwambie atulie maisha cio papara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…