Habari za leo wanaJF,
Napenda kujua ni software zipi zinazotumika katika kucheza na vocal za wimbo.
Ninaposema kucheza na vocal za wimbo namaanisha kuweka effects katika wimbo mfano auto tune ya t-pain, kuweza kuseparate vocals na instrumental katika wimbo na kuzisave kama mafile tofauti...n.k
Mfano mzuri ni katika mixtracks mbalimbali tunazosikia. utakuta watu wanafanya remix zao..wanachukua verse katika wimbo wa msanii kama jay-z alafu wanaweka hizo vocal zake katika beat ya wimbo wa msanii mwingine..yani kama hujui verse unaweza ukasema nyimbo ni mpya..
ningeomba mnitajie software zinazoweza kufanya hivi vitu na jinsi ya kuzipata..kama zinaweza kupatikana for free pia nitashukuru ukiniambia jinsi ya kuzipata ili niweze kujifunza kidogo...
Tafuta virtula dj pro v6.5, ina hizo plugins, ila ukitumia v7 home freee deition haina hivyo vitu. Hiyo utaweza kuingiza hata scratches na effects kibao.
Zile vocal hua zinatafutwa separate mzee,sio kwa kufuta futa beat..software tafuta cubase,fl studio,sound forge zote unaweza fanya hivyo vitu,but plugins hua zinatafutwa nje ya software..tafuta on google,VST audio plugins zitakupa info
Ukike uko wapi hapo kwenye hiyo post ya jamaa?yeye kuomba msaada au kuomba msaada kuhusu software au kushindwa kugoogle?jiheshim na sio lazima ucomment kwenye kila post.