Wanajamvi Msaada kwa yeyote anayejua qualification za kujiunga na kidato cha tano kwa matokeo ya BRN,Mara ya kwanza ilikuwa C tatu tu,sasa C imeshuka thamani,madogo wanaingiaje?
Sema unahitaji kujua sifa za kujiunga na K5' wala usiingize utani kwa kuweka sifa za BRN, kwa kuwa hizo hazipo. Sifa kujiunga na K5 kwa watahiniwa wa shule (gov na Private) ni Kama ifuatavyo:
1. Awe amepata daraja la siyo chini ya Credit (awali lilijulikana Kama Div.III),
2. Awe anaufaulu wa angalau masomo 3 kwa credit Pass, yaani A, B+, B na C, na
3. Awe amefaulu masomo yake ya tahasusi (combination) anayotaka kwenda kusoma, ufaulu usiopungua D kwenye masomo yote.