Usipoteze muda kukariri syntax, ni wastage of time, wewe muda mwingi tumia kujifunza core language na how to program, syntax ni kitu ambacho kitakuja automatically kwa sababu utakua unarudiarudia mara kwa mara, ukikwama you can always go back and search for the syntax, hadi itakaa tu kichwani, so usiimbe syntax ka ngonjera.
Kuhusu kusoma watu tunatofautiana, wengine ni wagumu kuelewa hadi kuelekezwa so video zinasaidia, wengine wanadive into the books moja kwa moja na wanajikuta wanaelewa, swala ni kutafuta what works for you na kustick nacho.
Mazoezi unayotafuta wewe sijui ni yapi hasa, ila kama umesema unasoma Java kwa ajili ya android application, kwa nini usitengeneze app kama zoezi lako la kwanza?
Mfano, umemaliza kusoma how to create a layout, activities, fragments, unajua kudeal na listeners, how interfaces na abstract classes work, unaweza jipima kwa kujaribu kutengeneza app kama ya kutunza contacts, mtu anaregister new contacts inatunza kwenye sqlite database na kuretreave hizo data baadaye, unaweza include na picha pia, email e.t.c. Na kuifanya even more complex unaweza ongeza data kama kupima calls mtu alizopiga kwa namba flani.
Kitu kama hiki unaweza ukahisi hujui lakini the moment ukianza, ukishindwa unagoogle majibu yanakuja fasta, read code, write code, utajikuta umefika mbali sana. Kusoma tu all the time bila kutengeneza kitu chako mwenyewe nadhani ndio sababu upo hadi leo unalalamika syntax hazikai kichwani.