Jinsi ya kutengeneza Mpango biashara ( Business Plan)

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
275
262
Katika dunia ya sasa utengenezaji wa mpango wa biashara umekuwa ni lazima na kwa biashara yoyote unayoifanya bila kuitengenezea mipango haiwezi kufanikiwa, leo nimeamua kuanza na baadhi ya mambo ambayo unatakiwa kuyafahamu unapotaka kutengeneza mpango wa biashara .

Hapa chini vifuatavyo ni vitu muhimu unavyotakiwa kuvizingatia katika utengenezaji wa mpango biashara wako, andika kwa umakini kiini cha wazo lako la biashara na lijumuishe vitu kama.

1/ Jina
2/ Aina ya biashara
3/ Historia ya biashara na maendeleo yake
4/ Huduma /bidhaa
5/ Tathmini ya Soko
6/ Ushindani
7/ Masoko
8./Ufanyaji kazi
9/ Usimamizi na utawala
10/ Uwezo wa wafanyakazi
11/Matatizo na utatuzi
12/ Maelezo ya kifedha

Jina na aina ya biashara

Kipengele cha kwanza na cha pili ni kama vinashabihiana kwanza ni inatakiwa uandike jina la biashara unayotegemea kufanya ( hapa sio aina ya biashara) ni jina linalokutambulisha wewe katika biashara , Pia hapa napo kuna tatizo majina ya biashara pia ni ishu haitakiwi kujichagulia tu ilimradi jina lako unaitwa Musa basi jina la biashara litakuwa Musa Genereal Enterprises uchaguzi wa jina la biashara nao unanafasi yake katika kuvuta wateja kwenye biashara yako. Ukimaliza hapo unaainisha sasa na aina ya biashara unayofanya je? Ni kutoa huduma au bidhaa kwa maelezo ya kujitosheleza.

Historia ya Biashara na maendeleo yake.
Sababu ya kuelezea hii ni kuangalia utungaji na nafasi yako katika soko pia maendeleo ya hiyo biashara, hapa unatakiwa utoe maelezo ya Taarifa za kuanzisha,uzoefu na uwezo wa mmiliki, Eneo, Matatizo na utatuzi wa matatizo yanayoendelea, uwekezaji wake, Mipango na Malengo ya baadae, Taarifa na muonekano wa soko, Washindani wakubwa na faida ya Bidhaa /huduma yako.

Huduma au bidhaa

Unatakiwa kueleza au kutoa maana ya bidhaa au huduma ambazo zinavutia kwa biashara yako.kwa kuzingatia maelezo ya utofauti wako,uwiano wa soko,Hatua ya uboreshaji wa huduma/bidhaa, uzalishaji, vitendea kazi( wafanyakazi na rasilimali ), fedha inayohitajika, Mzunguko wa uhai wa huduma/biashara na ukuaji wa baade.

Tathmini ya Soko.
Kuangalia bidhaa/ huduma na uhusiano wake na mtumiaji, vitu unavyotakiwa kuvielezea ni Soko unalolikusudia, watumiaji wake tabia zao,vitu vinavyotakiwa kwa huduma /bidhaa yako, majibu ya mtumiaji baada ya kutumia,sababu za kimasoko na msimamo wake, upenyo katika soko, Kuchangia soko,utafiti na kusoma,gharama na mpango wa mauzo.

Ushindani

Unatakiwa uanishe na kuelezea washindani wako na wewe mwenyewe ili mbinu zako ziwe imara baadi ya maelezo unayotakiwa uyatoe kwenye mpango biashara wako ni pamoja na Kujua washindani wako,taarifa za washindani, uwiano wa bidhaa /huduma, uwezo na udhaifu wa bidhaa /huduma, maendeleo ya baadae ya huduma/bidhaa na kinachohitajika sokoni

Uzi huu utaendelea kwa kumalizia vipengele 6 (sita) vilivyobakia,pia unaweza kuangalia matoleo mengine kuhusu ujasiriamali na biashara kwa kutembelea Elisha Chuma
 
Nahitaji kuanzisha kanisa, litakuwa na waumin wasio pungua sabini. Mtaji nina shiling 5Ml,
Nimepata kiwanja maeneo ya kimara, siku za ibada kwa wiki zitakuwa mara nne, ijumaa utkuwa mkesha. Kadrio la sadaka kwa mwezi ni shiling 2.5ml.nitakuwa na wahudumu 8 ambao wawili watafanya kazi ya kupepea wagonjwa , watatu kazi yao itakuwa ni kubeba wagonjwa, mmoja kupiga gitaa,
Vifaa ninavyoanza navyo, ni speaker kubwa tatu, gitaa mbili ,vipaza sauti vitatu na viti vya plastic 100,
Jina la kanisa bado nafikiria na katika hilo wana JFmtanisaidia,
Note, ni maneno ya kijana mmoja aliyekuja kuniaomba msaada wa kujiajiri baada ya maisha kuwa magum mtaani.
 
Katika dunia ya sasa utengenezaji wa mpango wa biashara umekuwa ni lazima na kwa biashara yoyote unayoifanya bila kuitengenezea mipango haiwezi kufanikiwa, leo nimeamua kuanza na baadhi ya mambo ambayo unatakiwa kuyafahamu unapotaka kutengeneza mpango wa biashara .

Hapa chini vifuatavyo ni vitu muhimu unavyotakiwa kuvizingatia katika utengenezaji wa mpango biashara wako, andika kwa umakini kiini cha wazo lako la biashara na lijumuishe vitu kama.

1/ Jina
2/ Aina ya biashara
3/ Historia ya biashara na maendeleo yake
4/ Huduma /bidhaa
5/ Tathmini ya Soko
6/ Ushindani
7/ Masoko
8./Ufanyaji kazi
9/ Usimamizi na utawala
10/ Uwezo wa wafanyakazi
11/Matatizo na utatuzi
12/ Maelezo ya kifedha

Jina na aina ya biashara

Kipengele cha kwanza na cha pili ni kama vinashabihiana kwanza ni inatakiwa uandike jina la biashara unayotegemea kufanya ( hapa sio aina ya biashara) ni jina linalokutambulisha wewe katika biashara , Pia hapa napo kuna tatizo majina ya biashara pia ni ishu haitakiwi kujichagulia tu ilimradi jina lako unaitwa Musa basi jina la biashara litakuwa Musa Genereal Enterprises uchaguzi wa jina la biashara nao unanafasi yake katika kuvuta wateja kwenye biashara yako. Ukimaliza hapo unaainisha sasa na aina ya biashara unayofanya je? Ni kutoa huduma au bidhaa kwa maelezo ya kujitosheleza.

Historia ya Biashara na maendeleo yake.
Sababu ya kuelezea hii ni kuangalia utungaji na nafasi yako katika soko pia maendeleo ya hiyo biashara, hapa unatakiwa utoe maelezo ya Taarifa za kuanzisha,uzoefu na uwezo wa mmiliki, Eneo, Matatizo na utatuzi wa matatizo yanayoendelea, uwekezaji wake, Mipango na Malengo ya baadae, Taarifa na muonekano wa soko, Washindani wakubwa na faida ya Bidhaa /huduma yako.

Huduma au bidhaa

Unatakiwa kueleza au kutoa maana ya bidhaa au huduma ambazo zinavutia kwa biashara yako.kwa kuzingatia maelezo ya utofauti wako,uwiano wa soko,Hatua ya uboreshaji wa huduma/bidhaa, uzalishaji, vitendea kazi( wafanyakazi na rasilimali ), fedha inayohitajika, Mzunguko wa uhai wa huduma/biashara na ukuaji wa baade.

Tathmini ya Soko.
Kuangalia bidhaa/ huduma na uhusiano wake na mtumiaji, vitu unavyotakiwa kuvielezea ni Soko unalolikusudia, watumiaji wake tabia zao,vitu vinavyotakiwa kwa huduma /bidhaa yako, majibu ya mtumiaji baada ya kutumia,sababu za kimasoko na msimamo wake, upenyo katika soko, Kuchangia soko,utafiti na kusoma,gharama na mpango wa mauzo.

Ushindani

Unatakiwa uanishe na kuelezea washindani wako na wewe mwenyewe ili mbinu zako ziwe imara baadi ya maelezo unayotakiwa uyatoe kwenye mpango biashara wako ni pamoja na Kujua washindani wako,taarifa za washindani, uwiano wa bidhaa /huduma, uwezo na udhaifu wa bidhaa /huduma, maendeleo ya baadae ya huduma/bidhaa na kinachohitajika sokoni

Uzi huu utaendelea kwa kumalizia vipengele 6 (sita) vilivyobakia,pia unaweza kuangalia matoleo mengine kuhusu ujasiriamali na biashara kwa kutembelea Elisha Chuma

msaada wako ni bora,una tija
 
Nahitaji business plan ya biashala ya kutengeza wine(wine garage) kwa mwanza nyegezi, so intanigarimu sh.??? Kunitengenezea???
 
Karibu kwa yeyote anaehitaji kutengenezewa Mpango biashara mawasiliano ni 0684 047323

Karibu
 
Back
Top Bottom