likandambwa
Member
- Sep 16, 2015
- 18
- 0
Pole sana mkuu. Makampuni yanatofautiana na sio kila kosa lazima upewe onyo, kuna baadhi ya makosa ukifanya adhabu yake ni kuachishwa kazi japo hilo inabidi liwepo na liwe wazi kwenye mkataba wako wa kazi au kanuni na taratibu za mwenendo wa wafanyakazi wa hiyo kampuni.
Kama haujafanya kosa linaloangukia kwenye hayo yaliyoainishwa ambayo yatakufanya upoteze kazi, unaweza kuanza kutafuta wanasheria kwa msaada zaidi. Kwa kipindi cha miezi 7 kosa pekee ambalo lingekupotezea kazi ni utendaji wa kazi kwa sababu ulikua bado upo kwenye probation, na hapo ungeitwa nakuelezwa ni wapi uongeze bidii ili kuboresha utendaji wako.
Mkuu pole sana
Mimi hua naamini kila tatizo linalonikuta ni kwasababu MUNGU anajua mimi ndiye nitakayeweza kulihimili
Amini hivyo na kulingana na dini yako MUNGU atatenda!
Asante sana mkuu
Ila sipo kwenye kampuni, hata hvyo sikuwahi kufanya kosa lolote kama nilivyotangulia kusema
Kama nilivyotangulia kusema ni kwamba tangu nianze kazi sijawahi kuitwa kuhusiana na kosa au mwenendo wowote mbaya
Pia kwa mujibu wa mkatab wangu wa kazi ni permenent and pensionable ila kama ambvyo utaratibu wa serikali ningethibitishwa kazini baada ya mwaka mmoja kwisha wa probation
Nashukuru kwa ushauri
Kama umepewa barua ni lazima imetaja na sababu ya kuachishwa kazi na ni lazima itakuwa imetoa maelekezo ya nini ukifanye kama hukuridhika na uamuzi huo.
Nenda kwenye chama cha wafanyakazi unachochangia ukiwa na salary slip yako haraka sana maana kwenye mambi kama hayo ishu ya muda ni relevant.
Mkuu usikubali ipoteza haki ako kuna taasisi nyingi tu zinasimamia haki za wafanyakazi embu anza nazo hizoo utapata msaada serikalini alaf unafukuzwaje kazi kienyeji hivyoo mkuu naamini utapata haki yako tu
Ww unazingua, ulikuwa kwenye probation ukachukua leave ukute ulisingizia ugonjwa, nnavojua ukiwa kwenye probation yo nat etittld kuchukua leave, kama kwel ulikuwa waumwa bas umeonewa bt kama ulfanya ubishooo ili ule bata imekula kwako
Kaka maelezo yako yenyewe yanajikangana,bt sema upo serikali kuu au za mitaa au shirika la umma tuangalie jinsi ya kukusaidia.
Alafu toa information vzr na zote ilivyo tokea muda huu siyo mda wa kuficha chochote.usipokuwa makini hyo kazi utapoteza mazima.
Alafu jua huwa si rahisi kufukuzwa kazi serikalini lazima kuna vikao kama 3 viwe vimefanyika juu yako na bado wanakupa muda wa kukata rufaa.pia barua huwa inaelewa kuwa kutokana na kikao cha tarehe fulani..bodi ya ajira imekufukuza kazi kwa sababu hizi ! Pia kabla ya hapo na wewe lazima utakuwa umepewa nafasi ya kujitetea mbele ya bodi.
Mkuu hakuna ubishoo hapa
Nilivunjika mkono baada ya kupata ajali ya bodaboda wakati narud nyumbani kutoka kazini ambapo dreva aliongia mtaron nikarushwa
Nikaletwa dsm kwa ajili ya matibabu baada ya kupewa rufaa
Baada ya kufanyiwa opereshen nikapewa E.D ya wiki nne na ukizingatia mkono uliovunjika ni wa kulia kwa hyo haufanyi kazi vema
Nilivyorud kwa msimamizi wangu nikawasilisha ED lakn after 2 days nikaletewa barua ya kuachishwa kazi kutoka kwa mwajiri dsm
NB
IELEWEKE KUWA NINAFANYA KAZ MKOAN NA MWAJIRI YUPO DSM
HUKU KUNA MSIMAMIZI TU
Kuwa makini inawezekana msimamizi wako amekuchongea kwa mwajiri wako ndio maana ukalimwa barua ya kupoteza kazi.
Who knows bana binadamu hatupendani hasa katika maeneo ya ajira.
Hapo kuna mchezo mchafu umefanyika ambao msimamizi wake anataka kumuweka mbadala wake!So that is very bad ila kama ameeleza kweli,hakika atarudi kazini!