Msaada: Natafuta kazi

Msaada: Natafuta kazi

J Mbungi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Posts
269
Reaction score
74
Ukisoma maelezo yangu yote itakuwa zaidi ya kunisaidia-Ahsante!

Ndugu wana Jamvi,Naomba yeyote anayeweza kunisaidia kupata kibarua katika magari ya mizigo.Kama yanayochukua mazao Mikoani na bidhaa mbali mbali..Nimejaribu kutafuta kibarua kulingana na Proffessional yangu ya Utalii(Kama Hoteliar - Front Office operations Na "Tour Operators - Kama "reservations officer" ) NIMEKOSA.. Nina mwaka wa pili sasa Tangu nianze kutafuta kazi za jinsi hiyo,lakini sijapata japo ninauzoefu wa miaka12 katika Kazi hizo.

Nimetafakari sana,mimi kama mwanaume aliyejaliwa afya na Nguvu za kutosha Kabisa(Naweza kubeba kilo mia bila shida kabisa),Niliwahi kuweka kambi shamba( Bagamoyo nikifanya shughuli za Vibarua Shambani)..Lakini ni za msimu na matajiri wamekuwa wanatutelekeza shambani bila msaada..

Sasa nimeamua kutumia nguvu zangu kufanya kazi ya kunitoa jasho la halali wala siyo kumwibia mtu.

Nimechagua kutafuta kazi za Magari makubwa ya mizigo yanayosafiri,iliniweze kutumia muda wangu mwingi katika utafutaji tena mbali na familia yangu(ilikupunguza "Stress na Pressure " nilivyonavyo kutoka kwa mke wangu).

Mausiano na mke wangu yamekuwa mabovu sana ,baada ya kuteteleka katika kipato...Hivyo ni kazi ngumu sana kuendelea kuwepo kwenye mazingira anayo niona mara kwa mara tena bila msaada wowote ninaotoa mimi kama Msimamizi wa familia.

Nimekuwa navumilia Matusi kejeli na mambo kama hayo kutoka kwa mwenzi wangu,kwa kushindwa "ku-deliver" kama mume>>(Lakini itafika wakati nitakufa kwa stress..."Maana kumpiga,au kujibishana naye kwa matusi siwezi na sijawahi kufanya hivyo)...Ila nina hofu uenda uvumilivu ukanishinda siku nikaja kumuumiza..(Maana matusi na kejeli zote za ulimwengu huu nishapatiwa)..Lakini kwa vile nilikuwa..na bado naamini hivyo kuwa ipo siku nitajaaliwa kurejesha mambo katika mstari.."As long as" nipo napambana kwa kila hali ilikupata kipato halali.

Nahitaji kazi ya kipato chochote nakurudi na mahitaji ya muhimu nyumbani japo kila baada ya wiki....Nahitaji kujichanganya na mazingira tofauti na niweze kutokaa kizembe nyumbani huku nikiendelea kumtia hasira mwenzangu( Maana nikitoka asubuhi,utarajia nitarudi na chochote..Nikirudi jioni mikono mitupu huwa ni shughuli pevu)..Hata mimi huwa natamani nisirudi nyumbani ninapokosa cha kurudi nacho....

Aliyeguswa tunaweza kuwasiliana(Nitaweza kujitambulisha na kumpatia mawasiliano Kwa "Private Message"(PM),ya hapa hapa JF...Nadhani waungwana mtanielewa,maana ili jukwaa lina watu tofauti tofauti na wenye mawazo tofauti tofauti..Vinginevyo ningeweka kila kitu hapa...NIWASHUKURU NYOTE..!

NATAFUTA KAZI YA UKONDACTA MAGARI YAMIZIGO YAENDAYO MIKOANI NA NJE YA NCHI/KUPAKIA NA KUSHUSHA NGUVU NINAZO:
 
Big up mkuu maisha ni safari ndefu kuna kupanda na kushuka. Mwanume ni kupambana tu mradi mkono uende kinywani kwa njia ya halali.
 
ugomvi ulionao na mkeo mnaweza mkautengeza ukawa mtaji na ajira kubwa na yenye kuwalipa vizuri.tafuta sababu zinazokufanya ugombane na mkeo,halafu tafakari sababu zingine zinazoweza wagombanisha wanandoa then fanya critical thinking ya majibu yake.majibu utakayopata yafrem vizuri na pamoja na sababu,then katafute mtu yoyote mwenye ukumbi muombe kuwa unataka kufanyia semina kwake ila gharama ya vyakula na vinywaji ataweza kiviandaa yeye na kuwauzia watu watakao kuja hapo.bandika matangazo sehemu mbali mbali ambayo yataonyesha kuwa USEMINA MAALUMU JUU YA WATU WALIO KATIKA NDOA NA WANAOTARAJIA KUINGIA KWENYE NDOA.panga gharama zote pamoja na ya chakula na vinywaji then ongeza 5000 ambayo itakuwa kwa kila kichwa ambayo itakuwa faida kwako.utaanza kupata ishirini lakini jinsi utakavyoweza kujinadi ndivyo jina lako litakua na kuwa na wafuasi wengi.USOMI NI AKILI NA SI NGUVU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom