Msaada: Nahitaji kazi yoyote

Nyete

Member
Apr 20, 2016
58
125
Wakuu Habari Za J'pili!
Wakuu Nakuja Kwenu Kuomba Msaada, Nimejaribu Kutafuta Kazi Za Vibarua Kwenye Viwanda,makampuni Lakini Nimegundua Bila Kuwa Na Chochote Kitu Cha Kumpa Supervisor Imekuwa Ngumu Kupata Kazi,nami kupata Riziki Tu Ya Familia Imekuwa Shida . Wana Jf Naombeni Msaada Wenu Mnisaidie Kunipa/ Mniunganishe Na Mtu Anaeweza Kunisaidia Kibarua. Naamini Jf Ni Mahali Jamii Inapokutana. Elimu Yangu Ni Darasa La7 . Kazi Yeyote Ya Nguvu, Ama Isiyohitaji Elimu Kubwa Naweza.
Naishi

Dar Es Salaam
kunduchi
0655544795
Asanteni.
 
David Harvey

JF-Expert Member
Jul 17, 2014
1,821
2,000
kutokana na elimu yako kuwa ndogo nakushauri nenda kijijini ukalime mkuu/ujiajiri naamini utafanikiwa tu.
Lakini ukiendelea kukomaa na vibarua utateseka sana
 
Nyete

Member
Apr 20, 2016
58
125
kutokana na elimu yako kuwa ndogo nakushauri nenda kijijini ukalime mkuu/ujiajiri naamini utafanikiwa tu.
Lakini ukiendelea kukomaa na vibarua utateseka sana
mkuu nashukuru kwa ushauri wako. lakini pia kilimo bila mtaji wa pembejeo ni shida pia,
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,729
2,000
Wakuu Habari Za J'pili!
Wakuu Nakuja Kwenu Kuomba Msaada, Nimejaribu Kutafuta Kazi Za Vibarua Kwenye Viwanda,makampuni Lakini Nimegundua Bila Kuwa Na Chochote Kitu Cha Kumpa Supervisor Imekuwa Ngumu Kupata Kazi,nami kupata Riziki Tu Ya Familia Imekuwa Shida . Wana Jf Naombeni Msaada Wenu Mnisaidie Kunipa/ Mniunganishe Na Mtu Anaeweza Kunisaidia Kibarua. Naamini Jf Ni Mahali Jamii Inapokutana. Elimu Yangu Ni Darasa La7 . Kazi Yeyote Ya Nguvu, Ama Isiyohitaji Elimu Kubwa Naweza.
Naishi

Dar Es Salaam
kunduchi
0655544791.
0765544791
Asanteni.
Nenda Takukuru ukawachukulie hela za moto uwapelekee hao masupervisor baada ya hapo hao hao Takukuru watakusaidia kukuombea kazi
 
Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,431
2,000
Pole mkuu kwa kuchelewa kugundua kuwa kazi za siku hizi bila supervisor ni ngumu

Tena mwingine anakuambia mshahara wa kwanza ni wangu.. watu wabaya sana

lakini usijali utapata "inshaallah"
 
chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
4,894
2,000
Wakuu Habari Za J'pili!
Wakuu Nakuja Kwenu Kuomba Msaada, Nimejaribu Kutafuta Kazi Za Vibarua Kwenye Viwanda,makampuni Lakini Nimegundua Bila Kuwa Na Chochote Kitu Cha Kumpa Supervisor Imekuwa Ngumu Kupata Kazi,nami kupata Riziki Tu Ya Familia Imekuwa Shida . Wana Jf Naombeni Msaada Wenu Mnisaidie Kunipa/ Mniunganishe Na Mtu Anaeweza Kunisaidia Kibarua. Naamini Jf Ni Mahali Jamii Inapokutana. Elimu Yangu Ni Darasa La7 . Kazi Yeyote Ya Nguvu, Ama Isiyohitaji Elimu Kubwa Naweza.
Naishi

Dar Es Salaam
kunduchi
0655544791.
0765544791
Asanteni.
ok, unaonekana una mwamko mkubwa wa kutaka kujikwamua kimaisha, lakini hjapitia kidato, lakini hii sio lazima hata
cha muhimu ili utoke ni mwamko na kujituma kwako, mimi nakushauri anza ufugaji unaweza ukakutoa vizuri tu
unaweza ukaanza kufuga kuku wachache ukakusanya fedha na kukuza idadi hadi kuwa na kuku wengi kabisa
kisha unatafuta tenda ya mahoteli au restaurant kuwa supply mayai na nyama
auunaweza ukafuga kitimoto pia
Lkini ufugaji ni fani inayohtaji elimu pia, itia nyuzi hapa jamiiforums zinazoelezea kuhusu ufugaji na kiimo pia ufanye na utafiti wako kivitendo kwa watu wenye uzoefu...UTATOKA
 
Nyete

Member
Apr 20, 2016
58
125
Nenda Takukuru ukawachukulie hela za moto uwapelekee hao masupervisor baada ya hapo hao hao Takukuru watakusaidia kukuombea kazi
Mkuu Kuwachukulia Hela Za Moto Za Takukuru Nadhani Pia Si Jambo Jema Kwani Wao Wameninyima Kibarua Tu Kutokana Na Nafasi Walizonazo, Hawakuninyang'anya Kitu. Hivyo Wakifungwa Ama Kufukuzwa Kazi Familia Zao Zitateseka Ni Bora Niombe Msaada Kwingine
 
Nyete

Member
Apr 20, 2016
58
125
Pole mkuu kwa kuchelewa kugundua kuwa kazi za siku hizi bila supervisor ni ngumu

Tena mwingine anakuambia mshahara wa kwanza ni wangu.. watu wabaya sana

lakini usijali utapata "inshaallah"
Nashukuru Sana Mkuu
 
MWANAMALEMBE

Senior Member
Jun 26, 2016
128
225
Nenda kwa mkuu wako wa mkoa RC Makonda akupe kazi! nimesikia anataka kuwatafuteni nyumba hadi nyumba msio na ajira.
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,729
2,000
Mkuu Kuwachukulia Hela Za Moto Za Takukuru Nadhani Pia Si Jambo Jema Kwani Wao Wameninyima Kibarua Tu Kutokana Na Nafasi Walizonazo, Hawakuninyang'anya Kitu. Hivyo Wakifungwa Ama Kufukuzwa Kazi Familia Zao Zitateseka Ni Bora Niombe Msaada Kwingine

Saidia mapambano zidi ya rushwa wewe, wewe mwenyewe ni muathirika wa rushwa halafu hutaki kuchukua hatua, unataka nani achukue hatua
 
Bhampupile

JF-Expert Member
Jul 6, 2015
811
1,000
Mie naona badala ya kuhangaika kutafuta vibarua ,, fikiria kwanza ni ufundi gani unapendelea,, kama ni wa magari,, kuchomelea vyuma,, udereva,, seremala,, ujenzi nk, sasa ni bora ukateseka kwa kipindi hiki kwa kutafuta sehemu ya kujifunzia huo ujuzi kwa watu binafsi,, baada ya mwaka au miezi kadhaa utaweza kupata ufundi wa kuendesha maisha yko,, vzr kuliko hivyo vibarua.
 
Nyete

Member
Apr 20, 2016
58
125
ok, unaonekana una mwamko mkubwa wa kutaka kujikwamua kimaisha, lakini hjapitia kidato, lakini hii sio lazima hata
cha muhimu ili utoke ni mwamko na kujituma kwako, mimi nakushauri anza ufugaji unaweza ukakutoa vizuri tu
unaweza ukaanza kufuga kuku wachache ukakusanya fedha na kukuza idadi hadi kuwa na kuku wengi kabisa
kisha unatafuta tenda ya mahoteli au restaurant kuwa supply mayai na nyama
auunaweza ukafuga kitimoto pia
Lkini ufugaji ni fani inayohtaji elimu pia, itia nyuzi hapa jamiiforums zinazoelezea kuhusu ufugaji na kiimo pia ufanye na utafiti wako kivitendo kwa watu wenye uzoefu...UTATOKA
nashukuru kwa elimu hiyo, ingawa kwa sasa bado nalia na kazi nipate mtaji kwani yote hayo uliyotaja,yanahitaji pesa.
 
  • Thanks
Reactions: BIR

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom