Msaada na ushauri juu ya sheria

Ti Go

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
942
919
Ndugu wana jamii forum nimepatwa na tatizo la kisheria ambalo ninaomba kwa anayejua namna ya kutoka anisaidie. Tatizo hili inawezekana lilishawapata wasomaji wa jamii forum, lakini hata kama halijapata mtu, inawezekana likaja na kwako kesho.
Nilikuwa na kesi na mtu nikampeleka mahakamani ya mwanzo. nikaleta mashahidi na yeye akaleta wa kwake. Kesi ikasikilizwa akashidwa na akahukumiwa kifungo. Alipokuwa gerezani akakata rufaa mahakama ya wilaya. Wakaona mbinu ya kumwokoa ni kubadirisha maelezo ya shahidi wangu mmoja ili yapingane na shahidi wa pili. Kwa kigezo hicho mahakama ya wilaya wakamwachia kwa kigezo kuwa ushahidi kwa upande wangu haujitosherezi kumfuga mtuhumiwa.
Swali langu ni kuwa kwa kuwa unapotaka kukata rufaa mahakama wanatumia ushahidi wa mwnzo na ushahidi wenyewe waliisha ubadiri nafanyaje. Kumbuka kuwa ili waweze kucheza na ushahidi niliomba nakala ya hukumu wakaichelewesha mpaka baada ya rufaa kukubaliwa. Je kuna uwezekano wa kuita mashahidi mara ya pili.
Kesi kama hii inawezekana haijawahi kutokea au pia inawezekana ikatokea siku za mbeleni. Tupeane uzoefu wa kisheria
 
Kwa ninavyojua sababu hujaridhika na kitendo cha mahakama kumuachia inabd ukate rufaa mahakama kuu sababu rufaa ya mwenzako ilikuwa mahakama ya wilaya...na katika kuandika sababu ya ww kukata rufaa ndio utasema kuwa ushahidi wako Wa mwanzo ulikuwa sahihi na unajitosheleza kwann mdai wako aachiwe? Mahakama yenyewe inaweza kuita mashahid upya kusikiliza upya ushahidi au ww muombaji unaeweza ukaiomba mahakama iite tena mashahidi kusikiliza upya. Na kitu kingine kuangalia time limit je uko ndan ya muda kukata rufaa?kama uko nje ya muda itabd uiombe mahakama extension of time to file an appeal out of time but with reasonable grounds for delay .
 
Nashukuru kwa kutenga muda wako kunipa ushauri. Mungu akubariki
 
Mkuu Ti Go hayo mambo yalishatokea sana tu. Kilichotokea ni kwamba mahakama ilipitia upya ushahidi uliotolewa na mahakama ya mwanzo (evaluation of evidence) na kuona kua uzito wa uhahidi haukuwa upande wako. Kiutaratibu mahakama iko sahihi. kama hukuridhika yakupasa kukata rufaa kwenda mahakama kuu. Huko, pamoja ma mambo mengine, wataangalia upya jinsi ushahidi ulivyotolewa na kuevalueti kuangalia uzito uko wapi. suala la kusililizwa upya kwa mashahidi hailpo, ingawaje kuna wakati mahakama inaweza amuru kuitwa kwa ushahidi flani ili kujiridhisha na kupata usahihi wa kesi zaidi. Sana sana hapo ukikata rufaa ni ngumu sana kwa ushahidi kuitishwa, kitakachofanyika ni kupitia tu kile kilichotolewa mahakama ya mwanzo.
 
Kwangu mimi naona kuna mapungufu katika zoezi zima la uendeshaji wa kesi. Wakati unatoa maelezo Hakimu ananakiri, kwako wewe siyo rahisi au hupewi nafasi ya kuhakikisha yale yaliyosemwa ndiyo yaliyoandikwa. Hakimu anaweza kunakiri kinyume ili kumsaidia anayetaka ashinde. Sijui kama naeleweka.
Katika enzi hizi, mahakama wangefanya kama ilivyo bungeni. Proceedings zikarekodiwa na machine - automation, ili ikitokea upotoshaji kumbukumbu irejewe kirahisi. Ni mawazo yangu
 
Kwangu mimi naona kuna mapungufu katika zoezi zima la uendeshaji wa kesi. Wakati unatoa maelezo Hakimu ananakiri, kwako wewe siyo rahisi au hupewi nafasi ya kuhakikisha yale yaliyosemwa ndiyo yaliyoandikwa. Hakimu anaweza kunakiri kinyume ili kumsaidia anayetaka ashinde. Sijui kama naeleweka.
Katika enzi hizi, mahakama wangefanya kama ilivyo bungeni. Proceedings zikarekodiwa na machine - automation, ili ikitokea upotoshaji kumbukumbu irejewe kirahisi. Ni mawazo yangu
Mawazo yako ni mazuri. Mahakama ya tanzania inao huo utaratibu wa kutumia mashine kirekodi proceeding (transcriber). hata hivyo kwa sasa, kutokana na ufinyu wa bajeti ni mahakama chache tu zinazofanya hivyo - mahakama ya rufani na mahakama kuu kitengo cha biashara. Kawaida hakimu anapoanakiri maneno anayoongea shaidi hawezi andika maneno yote, anaandika yale yenye uzito. Kama una wasiwasi na kinachoandikwa unao uwezo wa kuomba kupitia faili la kesi yako (case file perusal). Hii inaruhusiwa na utatakiwa kuripia ada.
 
Back
Top Bottom