Msaada: Mwanangu anasumbuliwa na vipele vyenye usaha

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,067
10,936
Habari wakuu,
Kijana wangu wa miezi nane anasumbuliwa na vipele ambavyo vinakuwa na usaha ndani. Vinamuwasha sana kiasi kwamba hawezi kulala na hata akilala basi atastuka muda mfupi.

Kwakweli ni mateso makubwa kwake. Nimempeleka hospitali akapata tiba ya muda mfupi lakini baada ya muda vinarudi.
63216a1cb6dc713a404ebcfaf0f49430.jpg

Naomba msaada wenu wakuu.
 
Pole mkuu, hyo hospital utaangaika sana jaribu dawa za kienyeji, kuna dawa moja wanakuaga nayo wamasai wanaiita ngesi,ipo kama ponje za mtama,unaisaga inakua unga unachanganya na maziwa fresh,hyo majibu yake ni siku3 tu.
 
jaribu kupaka dawa inaitwa BBE(BENZYL BENZOATE EMULSION),na sabuni ya kuogea atumie detol au tetmosal medicated soap na antibiotic ya maji kama ampiclox/azithromycine/cephalexin pia watibiwe members wengine wa family wenye tatizo kama hilo,pia nguo zake kama mashuka zifuliwe na mji ya moto na kupasiwa.MPELEKE HOSPITALI TATIZO LAKE NI LA KAWAIDA NA LINATIBIKA HOSPITALI/DISP KIURAHISI kupona kwa muda na kurudia inawezekana anapona alafu anaambukizwa tena na wenzake shuleni/nyumbani.MPELEKE HOSPITALI daktari atamchukua maelezo na kumtibu,na kama anatatizo lingine linaloloambatana atagundua kutoka kwenye maelezo ,uchunguzi na matokeo ya vipimo.
 
Habari wakuu,
Kijana wangu wa miezi nane anasumbuliwa na vipele ambavyo vinakuwa na usaha ndani. Vinamuwasha sana kiasi kwamba hawezi kulala na hata akilala basi atastuka muda mfupi.

Kwakweli ni mateso makubwa kwake. Nimempeleka hospitali akapata tiba ya muda mfupi lakini baada ya muda vinarudi.
63216a1cb6dc713a404ebcfaf0f49430.jpg

Naomba msaada wenu wakuu.
Anapandisha joto?
 
Yes, anapandisha joto wakati mwingine. Nampoza kwa panadol.
Hiyo ni Impetigo, ni serious infection ya ngozi (bacteria), inaweza leta compications nyingi zaidi, cha msingi nenda hospitali apewe huduma muafaka, si vyema kusema matibabu hapa sababu taaluma ya udaktari haisupport matibabu ya mtandaoni au simu (bila kumwona mgonjwa), dr atamwona na kuna vipimo atafanya vya kujiridhisha kuhusu magonjwa yanayoweza ambatana na huo ugonjwa, hivyo hapa nakupa ushauri uwahi huko.... homa katika hali hiyo ya ngozi si dalili nzuri.
 
Kwa watoto wadogo acha kutumia vyakula vyote vya supermarket ni hatari kwa ngozi na afya kwa ujumla, hvyo vipele vinapona lkn zingatia sana misosi ya supermarket, acha acha acha
 
Hiyo ni Impetigo, ni serious infection ya ngozi (bacteria), inaweza leta compications nyingi zaidi, cha msingi nenda hospitali apewe huduma muafaka, si vyema kusema matibabu hapa sababu taaluma ya udaktari haisupport matibabu ya mtandaoni au simu (bila kumwona mgonjwa), dr atamwona na kuna vipimo atafanya vya kujiridhisha kuhusu magonjwa yanayoweza ambatana na huo ugonjwa, hivyo hapa nakupa ushauri uwahi huko.... homa katika hali hiyo ya ngozi si dalili nzuri.
Nilienda jana kwa daktari wa watoto yupo Sinza Kijiweni (Dr. Emmanuel) vipimo vinaonesha ana blood infection. Nimepatiwa dawa ya kunywa, kuoshea na kupaka. Nasubiri nione kama atapona.

Pia nimeshauriwa kuacha kumpatia maziwa ya ng'ombe, Blue band, Tanbond, Samaki maji baridi.
 
Nilienda jana kwa daktari wa watoto yupo Sinza Kijiweni (Dr. Emmanuel) vipimo vinaonesha ana blood infection. Nimepatiwa dawa ya kunywa, kuoshea na kupaka. Nasubiri nione kama atapona.
Yupo sahihi.... tumia dawa
 
Nilienda jana kwa daktari wa watoto yupo Sinza Kijiweni (Dr. Emmanuel) vipimo vinaonesha ana blood infection. Nimepatiwa dawa ya kunywa, kuoshea na kupaka. Nasubiri nione kama atapona.
Hahahah mbona kama hujiamini? Mtoto atapona tu ukifuata masharti, usipo fuata atajiambukiza tena (reinfection), na hali itarudia tena
 
Wasiwasi muhimu mkuu, katoto kenyewe ndio hako hako kamoja roho yangu.
 
Back
Top Bottom