Kama nilivyoeleza hapo juu, mtoto wangu wa kike umri ni mwaka mmoja na miezi 4 amekuwa akigoma kula na kama akila basi ni kidogo sana napo hadi umlazimishe.
Tatizo linaweza kuwa nini? Na suluhisho la hili tatizo ni nini?
1: Watoto hawa wanaweza kuwa na shida nyingine ya kiafya.
2: Wakati mwingine ni tabia kulingana na umri.
3: Wengine ni mtindo wa maisha: tunaeapa maziwa na juice zenye sukari nyingi kitu ambacho huwafanya wawe na shibe na nguvu za kutosha na wadione haja ya na hamu ya kula.
NB: Wahusishe wataalamu wa afya kujua nini kinamsibu mwanao.