Habari wana JF,
Naomba msaada kwa wazoefu&wataalamu wa ujenzi wa nyumba kuhusu msingi wa nyumba.Je ni kweli msingi wa nyumba ya matofali ya kuchoma huwa unajengwa kwa kushindilia mchanga tu na kupanga matofali bila zege na nyumba ikadumu?
Naomba msaada wenu&mbarikiwe.
Nakushauri uwe makini sana na ushauri unaopokea hapa jukwaani, wapo wachache wanafahamu ujenzi na walio baki wanachangia kwa mazoea hasa walivyoona au kusikia ujenzi ulivyo. ikiwa utachukuwa kila ushauri utahombana na fundi wako bure.Asanteni sana kwa msaada wenu.Nyumba najengea maeneo ya morogoro
mkuu bila shaka huna uzoefu na ujenzi.Hiyo itakuwa si nyumba ya kudumu ama hali ya uchumi iwe hairuhusu maana watu wanajengaga nyumba ya udongo kila kuanzia chini hadi juu...Ila kama mtu unataka kujenga sidhani kama kuna fundi mwenye uwelewa anaweza kukujengea nyumba imara kwa njia hiyo ulioiainisha...
kwa swali hilo wew wajua ujenziunaijengea ukanda gani, tukupe soil characteristic ya ukanda huo ndio ujue msingi unakuwaje!?
Msikilize fundi anasema nini mimi si mwenyeji wa huko morogoro lakini kuna ndugu yangu anaishi ifakara nyumba yake nayo ilijigengwa kwa mtindo huo nadhani wenyeji wa huko wanauzowefu na huo ujenzi wa aina hiyo.Ni hivi,fundi anasema kuwa msingi sio lazima niweke zege,ameshauri kuwa msingi ukishachimbwa ashindilie mchanga halafu aanze kuweka tofali.Zege niweke kwenye linta.
Mimi pia fundi wangu kanishauri nisimwage zege nichimbe mzingi halafu nishindilie mchanga kisha nijengee tofali za block kama coz tano kisha niendelee na tofali za kuchoma. Naombeni ushauri pia wana JF najengea DodomaNi hivi,fundi anasema kuwa msingi sio lazima niweke zege,ameshauri kuwa msingi ukishachimbwa ashindilie mchanga halafu aanze kuweka tofali.Zege niweke kwenye linta.